Nyumba Inauzwa Mbezi Beach 150mil

Kitomai

JF-Expert Member
May 21, 2009
1,062
299
Ina vyumba vitatu. Ipo katika kiwanja chenye ukubwa wa 400 sqmts. Kiwanja chake kina hati miliki. Ipo katika barabara kubwa inayoonganisha barabara mbili kubwa...New Bagamoyo road na Mwai kibaki. kuelekea katika nyumba unaingilia Mbezi Beach Makonde na ipo karibu na Esacs secondary school. Kuiona tuwasiliane kupitia simu hii 0784225000.

IMG_0271.JPG
IMG_0272.JPG
 
Mkuu naomba kupata location exactly ni sehemu gani?mbezi ya Chini au mbezi afrcana au Salasala?
 
Lau kama Mungu angefahamu kwamba bahari zake wanadamu watazitumia kuongeza neno "beach" kwenye maeneo yao na na kutaka kuyauza kwa bei zinazomchukiza yeye; wallah tena nadhani Mungu angezifanya beach ziwe maeneo ya kuchukiza yasiyofaa kuishi ili zitumike tu kwa shughuli za uvuvi tu na usafiri!!

400 sqm = TZS 150 Million!

Halafu si ajabu hata mimi ningekuwa na hiyo 150M huenda nami ningenunua kwa sababu kuna neno "beach!"

Mimi sio mfanyakazi wa serikali lakini potelea mbali wacheni tu nihamie Dodoma niwaachie akina Bashite Dar es salaam yao!!!
 
Mm naona hakuna nyumba hapo unauza kiwanja tu tena 150 milioni kwa 400 square metres!!!
 
Napata ukakasi kwa hili tangazo. Mbezi beach mil 150? Tena Makonde!
 
Mkuu masikhara sasa hayo. Tuambie unauza kiwanja siyo nyumba
 
YAANI NYIE MNASHANGAA HIYO BEI KWA MBEZI BEACH ? AU MNALINGANISHA NA BEI ZA TABATA KIMANGA AU CHANIKA YETU ? POLENI SANA.
 
Njaa mbaya sana, nyumba kaijenga mwenzako kipindi wewe hujitambui kabisa leo unataka kutoka kirahisi hivyo.Umelotea njia fanya kazi halali.Madalali wa mtaani they are too sharrow, .Hivi 150 ml. unajua nyumba za kawaida zenye hadhi unapata 3?
Hupati mteja ng'o kwaajili ya tamaa zako.
Siku hizi ukimwona mtu kanunua kiwanja au nyumba zaidi ya ml. mia ujue kalipenda eneo kwa shughuli zake za uwekezaji na so rongorongo zako hizo. Acha tamaa uta....
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom