Mkuu hawa wenye nyumba muwaambie/muwashauri, nyinyi kama madalali wao, wabadilike.
Ni ngumu sana siku hizi kumdai mtu kodi ya miezi sita au mwaka. Ingawa ni kweli nyumba ni yake na hapangiwi, Lakini reality huku mtaani ni tofauti. Ni vema hata wakafanya miezi mitatu mitatu!
Tusifanye biashara kukomoana. Sheria ya kuwabana wapangishaji na wapangaji iko jikoni, Mh. Lukuvi anaiandaa. Kodi itakuwa ni mwezi mmoja mmoja. Na madalali itabidi mlipe kodi. In fact nchi nyingi duniani, kodi ni mwezi mmoja mmoja. Hii ya kulipa mwaka mzima ...ni Tanzania tuu na ni kwasababu zilikuwa hela nyingi za kifisadi mtaani. Sasa hivi JPM ametubana tuishi kwa jasho!
Wahusika wabadilike!