Nyumba inapangishwa Kigamboni

Nyumba inapangishwa Kigamboni

Family Hammer

Member
Joined
Mar 20, 2015
Posts
6
Reaction score
4
Nyumba mpya inapangishwa ipo Kigamboni maeneo ya Kibada.

Nyumba ni self cointained, ina vyumba vitatu, kimoja ni Master. Sebule, jiko na sehemu ya kulia. Kuna choo na bafu vinavyojitegemea.

Kama inavyooneka kwenye picha finishing ipo ukingoni, Mteja anaweza kupendekeza rangi na vionjo vingine atakavyopenda nimwekee.

Kwa maelezo zaidi tuwasiliane kwenye namba +255 767 629999

20150320_112139.jpg




DSC02322.JPG DSC02287.JPG DSC02290.JPG


20150403_105625[1].jpg 20150403_105333[1].jpg 20150320_112139.jpg
 
Ndugu, nisaidie kufanahamu.Hapo umetumia sh ngapi mpaka kufikia hapao ilipo.
 
Umetumia muda gani? unakisia kama sh ngapi? Unajua wengine tuanogopa kwani vipatu duni Ila tukipata mfano kama wako mtu unaweza kukadilia?

Asante
 
Bosi natumaini una kiwanja,na kama una malengo ya kujenga natumaini hakuna kitu ambacho kitashindikana hapa chini ya jua. Ni wewe tu kujiamini ya kwamba unaweza. Watu wengi waliojenga walianza mdogo mdogo mpaka sasa wamemaliza nyumba zao.

Hatua za Ujenzi.

1. Ramani, tafuta ramani ambayo unaipenda

2. Msingi, hii ni hatua muhimu sana katika ujenzi na nilazima msingi ujengwe kwa umakini zaidi ili kuepuka matatizo hapo baadae maana msingi ukiwa mbovu hata nyumba haitakua imara. Mahitaji ya ujenzi wa msingi ni mchanga, kokoto, matofali, cement, nondo n.k Kwenye jedwali hapo chini nitakupa makadirio ya haraka ya nyumba yangu na bei zinazotembea eneo hili. Hila gharama zinaweza kuzidi au kupungua kutegemea eneo ulilopo, aina ya nyumba unayotaka kujenga, site ilivyokaa nk.

Bosi, hizo gharama chini wala si zisikutishe. Kama vipi unaweza ukanunua vitu kama tofali, mchanga na kokoto ukamwaga site huku ukiendelea kutafuta hela ya material zinginezo.

Bosi, Ukifanikiwa kujenga msingi unakuwa umepiga hatua muhimu sana.

Item
Unit price
Cost
Mchanga tripu 2
130000/=
260000
Kokoto tripu 2
300000
600000
Matofali 2000
1050
2100000
Nondo

1000000
Labour charge

1500000
Bending wire, misumari, mbao, transport n.k

1000000
Total

6460000

3. Kusimamisha boma,hapa ndio nyumba inaanza kuonekana. Kwa nyumba saizi ya kati unahitaji tofali kama 2000, nondo kwa ajili ya beam, kokoto n.k

4. Kuezeka na Kupaua, gharama itategemea na unataka kupaua kwa material gani. Ni kugumu kidogo kwakuwa ni lazima kufanyika awamu moja.

5. Kushimba mashimo ya maji taka, blundering, wiring, plumbing,kuweka milango na madirisha, plaster etc. hii ni hatua ambayo unaweza kwenda nayo mdogo mdogo.

6. Finishing, Hatua ya mwisho ya kuipamba nyumba yako kwa rangi, makabati, sink, tiles nk. Hapa itategemea wewe unataka nyumba yako iweje na mfuko wakati huo unasemaje. Uzuri unaweza kwenda mdogo.

Bosi nadhani nimekupa mwanga, ingawa kuna vitu vingi nimeviacha vinaelea hewani. Natumaini wanajamii wengine wanakuja kuchangia.
 
Family Hammer,
wewe umeshuka Data zoote,ila mambo muhim unayotakiwa kueleza kuhus nyumba unayouza umekwepa.
Maswali ni mawili tu hapa
a)Bei Gani
b)Ukubwa wa kiwanja ni upi
c)Je kiwanja kimepimwa?
d)Kigamboni kubwa,je Kigamboni ipi?
 
Family Hammer,
wewe umeshuka Data zoote,ila mambo muhim unayotakiwa kueleza kuhus nyumba unayouza umekwepa.
Maswali ni mawili tu hapa
a)Bei Gani
b)Ukubwa wa kiwanja ni upi
c)Je kiwanja kimepimwa?
d)Kigamboni kubwa,je Kigamboni ipi?

Rudia kusoma uzi upya Mkuu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom