Nyomi za wanasiasa ushahidi wa umasikini wa nchi

Phillipo Bukililo

JF-Expert Member
Dec 29, 2015
18,487
13,612
Wakati wa kampeni za uchaguzi, kuliibuka tabia ya wanasiasa kufurahia wingi wa watu waliokuwa wakiwasikiliza wagombea. CCM wakifanya mkutano unaojaza watu, baadhi ya wanachama wakawa na tabia ya kuchukua picha na kuziweka mtandaoni. UKAWA nao hawakubaki nyuma, walizitupia picha nyingi kwenye facebook. Na wote wanaoweka picha zinazoonyesha wingi wa watu walijaribu kujenga kuwa vyama vyao vinapendwa na vitashinda uchaguzi kwani ushahidi ni hizo picha zao.

Uchaguzi umekwisha lakini kitu kimoja ambacho ndio sababu haswa ya wingi wa watu katika mikutano ya kampeni, bado hakijaisha na hakiwezi kumalizika kirahisi tu, naongelea umasikini. Mtu ambaye alikuwa tayari kukaa juani kuanzia saa tano asubuhi pale Jangwani, wakati mgombea urais anaanza kuhutubia saa kumi jioni, anayo matumaini makubwa, anazo ndoto nyingi za kimaendeleo. Wanasiasa kwa ujumla wao na hata wale waliokuwa wakiweka picha za wingi wa watu, huu sasa ndio wakati wa kufikiria kwa undani jinsi ya kukitekeleza kile kilichoahidiwa.


Nyomi (wingi wa watu) ni kielelezo cha umasikini wa Taifa letu. Huwezi ukamuweka juani Mmarekani au Muingereza kwa masaa matano eti kwa nia tu ya kumsubiri mgombea urais. Nyomi ni kielelezo cha kukata tamaa kimaisha, ni kielelezo cha ukosefu wa kazi, ni kielelezo cha watu wanaoishi maisha ya ubangaizaji. Huu uwe ni wakati wa kupunguza mawazo ya siasa, kwani hazijawahi kuwa na baraka kwa maisha ya walio wengi.

Waliofurahia nyomi na kudhani kuwa ndio kukubalika kwa vyama vyao, ukweli ni kwamba kazi iliyopo ni nzito sana. Nawatakia mafanikio wanasiasa wetu ili waweze kukidhi matarajio ya nyomi wakati wa kampeni.
 
Back
Top Bottom