Stabilaiza
JF-Expert Member
- Jul 11, 2012
- 1,843
- 1,143
Kuomba msamaha ni uungwana hivyo itakuwa jambo jema kwa Mzee Mwanakijiji a.k.a. MMM, kuwaomba msamaha wananchi wazalendo kwa kuchangia kuwavimbisha kichwa utawala uliopo madarakani hivi sasa.
Bila kujali ukandamizaji wa demokrasia katika nchi yetu tangu awamu ya tano ilipoanza , MMM ambaye hapo zamani, kwa kupitia maandishi yake mbalimbali aliweza kuibua uozo katika serikali ya CCM, aliwashangaza na kuwaacha midomo wazi watu wengi, kuwa mtu ambaye alidhaniwa kuwa mzalendo na mwana-demokrasia wa kweli amegeuka na kuitetea waziwazi serikali inayokandamiza demokrasia na uhuru wa kujieleza. Kwa uelewa wa MMM, anafahamu fika kuwa huwezi kutenganisha demokrasia na maendeleo.
Msingi wa maendeleo ni fikra huru za mwanadamu. Uhuru wa kufikiri, kuamua na kusema ni haki ya kuzaliwa. Hivyo, inatosha kwa mtu wa uelewa hata wa kawaida kung’amua kuwa kutetea utawala unaokandamiza demokrasia ni kutetea utawala unaodidimiza maendeleo.
Binafsi, sielewi MMM alitumia busara gani kuutetea utawala huu ambao hata mwananchi wa kijijini anaona kuwa ni mbovu. Baada ya kuvimbishwa kichwa na baadhi ya watu, akiwemo MMM, utawala wa Magufuli ulizidisha kasi ya kudidimiza demokrasia na ukandamizaji wa haki za raia.
Mifano michache ni pamoja na kuzuia mikutano halali ya vyama vya siasa, kutukana wananchi, kufukuza wafanyakazi wa umma bila kufuata utaraibu (kwa mfano kuwauliza wananchi katika mkutano wa hadhara, nimtumbue au nisimtumbue?) Ni baada tu ya kuguswa kukamatwa kwa mwanaharakati nguli wa mtandao maarufu wa kijamii na kupotea kwa Ben Saanane, ndiyo MMM ameanza kuonekana kusituka kidogo japo hajarejesha makali yake yaliyozoeleka ya kutetea demokrasia na kupinga ukandamizaji.
Sasa, tunamtaka MMM, aonyeshe uwajibikaji kwa kuwaomba msamaha wananchi kwa kupotoka kwake na kushadidia utawala ya uwamu na hivyo kuendelea kudidimiza demokrasia na kukandamiza wananchi. Na hii ni nyingine ya kufungia mwaka.