fakhbros
JF-Expert Member
- Sep 14, 2013
- 384
- 657

Wimbo ulikuwa ukiimbwa hivi-
Mwenzenu mie najuta"
Nilikuwa na Mpenzi wangu Maprosoo
Aliniahidi tutafunga ndoa
Yakweli, Namapumziko yetu yangekuwa Mombasa
Amanipa ujauzito na sasa miezi sita yapata Simuoni,
Ehh Maprosooooox2
Wazazi na nyumbani, Wamenifukuzaa
Hata chumba changu, Wamepangisha sababu yako maprosoo×2
Hata Anko ataki kuniona sasa nikwende wapi ehee
Eyooooo----
Ehh Maprosoooo
Hizi zilikuwa nyimbo za wakati ule maprosoo alikuwa anaeleweka
Mwanamke alikuwa akihongwa mia inakuwa ndio harusi yake
Maprosoo walikuwa ni watu makini sio kama maprosoo wakileo ambao wanataka kulelewa na shuga momy
Enzi hizo bwana na kiatu chako cha raizoni, Suruali ya Bugaas, ukichomekea razima upigilie tai nyeusi
Mkononi ungeweka saa ya motima au Seiko...
We acha vijana wa kileo hata kuimba wanabana vipua vyao tu sauti hazitoki unaweza kudhani scania inapanda kitonga
We maprosoo hebu tukumbushane wazee wenzagu
Kuna wimbo kama wa mbaraka mwisheh
Sasa nimehamia mtaa wa saba, sio kule niliko ishi zamani kila siku paka hawaishi kulia lia
Nyumba ile sio nyumba ilikuwa na mikosii eeh×2
Maprosoo hebu na wewe tafadhari weka wimbo wa enzi zako.....