Nyimbo gani zinaweza kurudisha mood yako sawa unapokuwa na msongo wa Mawazo? Your Inspiration songs?

Humble African

JF-Expert Member
Jul 28, 2013
4,779
14,377
Kimsingi kila binadamu anapitia kwenye mood swing kutokana na situation mbali mbali anazopitia na kusababisha awe down and hollow sometimes...sasa katika hali hiyo ya upweke na kuona mlima umekuwa mkubwa maishan mwako huwa ni nyimbo zipi zinaweza kupandisha morali na kuleta inspirational na positive view ya maisha tena?

Hii inatokana na trend ya watu kujiua Kwa kasi saana miaka hii ambapo nyuma ya pazia panagubikwa na visa na mikasa mizito na migumu tofauti tofauti ambayo wahusika wanakosa msaada wa kuyahimili magumu hayo na kuishia kujitoa uhai labda kwa kuweka experience na namna tulizotumia kuhandle hayo magumu yalipotufika inaweza kusaidia watu kadhaa wasipite kwenye njia ya bonde la uvuli wa mauti via kujiua, weka nyimbo au hata maneno ya kuuisha nafsi zilizopondeka na kukata tamaa.

Matter of fact, wataalamu wa muziki wameitimisha kwa tafiti kwamba muziki unaweza kuwa tiba yaani "music therapy" labda kwa upande wako yaliwahi kukufika magumu lakini kwa kutumia nguvu ya tiba iliyomo kwenye music therapy ukarecovery na kuendelea na maisha positively. Tungependa kusikia hiyo experience hapa jamvini.

Binafsi ngoma hizi zimekuwa msaada saana kwangu when I'm down, hollow, psychological exhausted, and pissed off.

Grace matata - free soul
Bob Marley - three little birds.
Joe purdy - wash away
Olivier mtukudzi - hear me lord
Lokua kanza - mutoto
Lokua kanza - Never lose your soul
Kelly clarkson - because of you
Zahara - loliwe
Zahara - Destiny
Passenger - whisper
Passenger - David
Babyface - How come how long
Celion Dion - all by myself
Julio iglesias - Starry starry night
Adele - I can't make you love me when you don't.

Hii ndio huwa maktaba inayoplay ninapokuwa emotional jammed na ninahitaji kurudi back to normal...kwako ni nyimbo zipi unazoplay unapokuwa unahitaji emotional inspiration? Pindi unapokuwa stressed up?
 
Screenshot_2017-01-28-23-14-36.jpg
 
Back
Top Bottom