Nyakati tofauti za mahusiano

Juandeglo

JF-Expert Member
Dec 20, 2014
1,023
2,726
Habari zenu nyote. Wakubwa shkamooni, wadogo kama kawaida!!

Naomba nielekee kwenye mada lakini naanza na mfano. Kuna mkoa huwa napenda kutembelea anytime katika mwaka. Nimeshatembelea mara mbili na hii ni mara ya tatu. Sasa kwa mara mbili nilizokuja nilikuta mti umekauka hauna majani. Nikajisemea ndani yangu..huu mti umekauka sa si waukate tu, hauna faida yoyote..hauna majani hauna lolote uko uko tu. Lakini hii mara ya tatu nimekuta mti umejaa majani tele. Nikajisemea loh..ungekatwa kivuli kingetokea wapi..nikapata somo timilifu katika mtazamo wangu.

Namquote mwana JF mmoja katika thread zilizopita kitambo sana. Alisema "love is hard, kuna wakati lazima mpitie majaribu katika mahusiano. Either distance misunderstanding au financial crisis."

So nimekuja kujifunza na kuelewa kuwa Love is not as the way its painted kwenye social medias, society, au fikra zetu (mmoja mmoja). Mapenzi yana nyakati. Kuna kiangazi, masika, kipupwe na Vuli. Kila mtu ana nyakati anayoipenda katika hizi nne..vivyo hivyo na mapenzi au mahusiano pia. Katika mahusiano from the start mpaka ndoa na mpaka kifo kuna nyakati tofauti. Kuna nyakati ambazo mahusiano yanakuwa matamu asikwambie mtu tu tu...yani hapo ukiambiwa lolote utasikia lakini hutaelewa because pale hisia zinakuwa high kinyama.

Movie hunoga kiangazi kinaposonga..haloo. unaanza kudoubt au this aint the person for me...mara nyingi hii hujitokeza kwenye muda wa preparations za ndoa na mnaweza ingia nayo ndani ya ndoa...usipokua makini unaweza ugome kuoa au kuolewa thinking "huyu si mtu sahihi kwangu, probably God is speaking to me" ngoja nimuache tu. Kumbe alikuwa sahihi sana tu.

Wanaume na wanawake jueni hili. Hakuna perfection duniani. Mara nyingi nasoma threads wanawake this wanawake that..ukijaribu kuchunguza katika familia yule mtoto ambae yuko fasta kusemea wenzake yeye ndo anakuwaga tatizo. (Jaza jibu). Lakini pia tuelewe jamani hakuna mkamilifu duniani. Lets learn kuishi na madhaifu ya kiumbe mwenzako. Kama huwezi kuishi na madhaifu ya mtu...utatangatanga mpk kifo chako. Kwa sababu kila mtu anayepumua ana kasoro.

Usipompata mchoyo mwenye upendo kwako, utampata mwenye gubu na roho mbaya ila mchakarikaji kwenye kuzisaka na sio bahili. Ni mimi na wewe kupima lipi unaweza kulibeba na kuishi nalo. Tubadilishe mtazamo tutapata the best out of life. Lakini ukitafuta kinyago (perfection) itabidi uchonge. Unaweza usipata mwanaume mwenye pesa lakini ana pa kuishi, anaamka asubuhi kutafuta hakosi fedha ya ugali na mboga na wewe una kidogo maisha yanaweza songa. Sio lazima uvae mashela sijui amapiano na Mc mkubwa..mnaweza enda apa kanisani afu mkala pilau kuku nyie na familia zenu afu ikawa imeisha mkafanya maisha. As long as ana spirit ya kupambana na anakupenda. He is sincere then go with it. Anaweza akose fedha ya kukupa saloon 50000 tafuta style cheap za kukupendezesha ili msaidiane mpige hatua kimaisha.

Times have changed..kama una upendo wa kweli kwa mwenza wako hakuna sababu itakayowazuia kufanya maisha. Muoane..mjijenge na mvumiliane..love requires effort asikwambie mtu masela.. tena from both sides. Na usianze kuona ooh sijui najitoa sana yeye hajitoi..ukishaanza kuweka thermometer kwenye mapenz jiulize je kuna upendo kwako?? Upendo haujivuni, hauhesabu mabaya..huvumilia yote, huamini yote..etc

Na huu ni mtazamo wangu.

#fullstopu#
 
Love requires effort maselaaa...naomba mnielewe masela wakike na wakiume.

wekezeni kwenye effort mtoa Uzi kasema.
 
Back
Top Bottom