Huyo air controller nafikiri hakulala vizuri na alitaka kusababisha ajali mbaya kwa uzembe. Hivi huu uwanja wa Barcelona bado una operate kwa mtindo wakizamani kama uwanja wetu wa Dar Es Salaam na Nairobi ambako runway ya kupaa na kutua inakuwa ni hiyo hiyo moja? Viwanja vya kisasa runway ya kutua ni tofauti kabisa na run way ya kupaa na hivyo kuondoa kabisa uwezekano wa uzembe kama huu kutokea.
Tiba
Unajua kuwa controller wa sehemu mbili, mmoja ni wa kupaisha na kushusha ndege na kundi jingine ni wale wa ku-Taxi ndege zikiwa kwenye uwanja. Hapa nafikiri ndipo palipotokea makosa kwa huyo jamaa wa kuongoza ndege zilizopo uwanjani akaielekeza vibaya ndege iliyokuwa ikitoka sehemu moja kwenda sehemu nyingine na hatujui walikuwa wanakwenda huko kwa sababu gani.
Nakubaliana na wewe kuwa viwanja vingi wanatenga kabisa. Pia sehemu ya ku-Taxi inafanyika pembeni kabisa mwa kiwanja. Sasa huyu ana Taxi katikati kabisa ya kiwanja?
Nasikia Schiphol Airport kuna Mkulima wa Mauwa huwa na yeye ana Taxi matrekta yake katikati ya barabara ya ndege. Ila huwa wanampa muda na wanamfungulia geti. Anakatiza kwa sekundi kadhaa na geti linafungwa,, uwanja unaanza tena kufanya kazi.
Mkuu hiyo ya Schiphol nafikiri ni exxageration tu. Pale Schiphol (wengine upaita Amsterdam) kuna sehemu ndege zinapishana na magari lakini kupishana kwenyewe ni kwamba barabara ya magari iko chini na juu ya hiyo barabara ni sehemu ya uwanja wa ndege ambako ndege zinapotua basi zikienda kupaki zinapita juu ya hiyo barabara. Sasa hiyo trekta na uwanja ule ulivyo busy, sijui.
Tiba
Nafikiri ni kweli. Hili niliambiwa na Prof. mmoja wakati tukiwa na somo la Airport Designing.
Sidhani kama alidanganya. Pia ukiangalia kwenye Google Map, utaona kuna barabara moja ambayo nafikiri inatumika tu ndege kupaa na iko kushoto kabisa mwa Airport na pale unaweza kweli ku-Cross na kama sikosei, huwa wana Cross kwani hata gate hakuna. Sijui kwa ulinzi wanafanya vipi. Uliyosema wewe, zipo hizo Viaduct kadhaa hapo Schiphol.
Gisborne Airport, New Zealand
It may be an understatement to say that Gisborne Airport on the North Island of New Zealand is atypical. This is because the Palmerston- North to Gisborne railway line cuts straight across the airport's main runway. Air traffic controllers must coordinate takeoffs and landings with train arrivals and although the rail line recently closed due to storm damage, the airport remains open and operates flights within the North Island.
Mkuu, huu uwanja ni mkubwa kiasi gani na airtraffic yake ikoje? Nafikiri huu uwanja na kama ule wa kwetu kule Kigoma ambako kwa siku inaweza kutua na kuruka ndege moja tu.
Tiba
Ukiangalia picha, nafikiri jamaa alitaka kufanya njia ya mkato, kama Waswahili vile.
Alitakiwa apite pembeni mwa uwanja na si katikati.....
Hapana some airports are designed in a way kua inabidi ukatize kwenye runway moja kwenda kwenye runway nyingine,kama julius nyerere ili uweze kwenda kwenye runway 05 inabidi ukatize runway 32/14 na inabidi upate clearance kutoka ATC, na pia ni responsibility ya rubani kuangalia kama kuna ndege yoyote inakuja on the base leg and final approach ndio avuke