Nusa nusa ya Magufuli kwa Kikwete

Donatila

JF-Expert Member
Oct 23, 2014
7,563
21,665
JK+pic.jpg

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Angella Kairuki amesema katika ‘nusanusa’ hiyo ukaguzi umeshaanza na utaangalia namna mabilioni yaliyokuwa yakitolewa na Serikali iliyopita kuwakopesha wananchi.

Dar es Salaam. Serikali ya Awamu ya Tano haitaki kuacha kitu chochote cha uongozi uliopita bila ‘kukinusa’.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Angella Kairuki amesema katika ‘nusanusa’ hiyo ukaguzi umeshaanza na utaangalia namna mabilioni yaliyokuwa yakitolewa na Serikali iliyopita kuwakopesha wananchi.

Amesema mabilioni hayo maarufu kwa jina la ‘Mabilioni ya JK’ yameanza kuchunguzwa namna yalivyoinufaisha jamii.

Chanzo: Mwananchi
 
Wengine watakuja kunusa zile milion 50 za kila kijiji.
Labda zingetolewa utawala mwingine!Thubutu mtu atie hapo mkono wake. Waulize watendaji wakati wa ujenzi wa madarasa kama waligusa pesa hizo.Uongozi unamatter sana!
 
Serikali ya Awamu ya Tano haitaki kuacha kitu chochote cha uongozi uliopita bila ‘kukinusa’.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Angella Kairuki amesema katika ‘nusanusa’ hiyo ukaguzi umeshaanza na utaangalia namna mabilioni yaliyokuwa yakitolewa na Serikali iliyopita kuwakopesha wananchi.

Mambo mengine yanashangaza sana.

Yaani utadhani nchi ilipinduliwa kijeshi. Au serikali iliyopo madarakani kwa sasa ni ya

chama kingine na si CCM. Ila chakushangaza wengi tu waliopo katika serikaliya awamu ya

tano walikuwa viongozi katikaserikali ya awamu ya nne. Waliyapongeza hayo

yaliyofanyika.
 
kuna mtu humu jf.
ameulizia na ile chench ya rada..

wangechunguza na hayo matumizi ya chenchi ya rada.
 
Vyakunusa haviwezi kuisha Nchi hii, na mbaya zaidi hata wakishavinusa hatusikii hata zzt.
 
Na zile pesa a.k.a mabilioni ya Muungano na Uhuru zilizopelekwa kienyeji kule Barabara ya Moroko Mwenge na Ghana Airport Mwanza nayo yanuswe nuswe
 
Wafufua makaburi at their best! Kairuki alikuwa naibu waziri tena wa sheria wa Kikwete na alikuwa kwenye proper position ya kumshauri juu ya mambo mengi aliyoyaona hayaendi sawa. Mkulu the same, pm the same also. Ni nini kinawaamsha leo na si jana? Bora wangefanya kimyakimya. Utendaji wa aina hii hautusaidii kuliondoa tatizo la mdororo wa uchumi. Wabuni style nyingine ya kuchapa kazi.
 
Nimechoka kusikia wakinusanusa, hiyo harufu imesha walewesha tiyari. Wawezaje mtu kushinda unafagia chooni halaf jioni yake useme ngoja ninuse harufu ka imekwisha??
Wote hao walikuwa wafagizi chooni hapo hapo, leo watanusa nini? Nadhani ni mbinu tu za kuua mabomu yalokuwa yakifyatuliwa na upinzani
 
Back
Top Bottom