NSSF yapigwa STOP kuanzisha miradi mipya, ni mpaka ripoti ya CAG itakapopitiwa

Bilionea Asigwa

JF-Expert Member
Sep 21, 2011
16,515
28,504
KAMATI ya Bunge ya Katiba na Sheria, imeagiza Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) kusitisha miradi yote mipya hadi hapo itakapopitia ripoti za Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) na kujiridhisha kama haina harufu za rushwa.

Akisoma taarifa ya majumuisho ya ziara ya wajumbe wa kamati hiyo waliyoifanya katika taasisi mbalimbali za Serikali, ofisi za mawaziri na mahakama jana, Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mohamed Mchengerwa, alisema wamefikia uamuzi huo baada ya kupitia miradi iliyopita na kubaini taarifa zake hazijajitosheleza.

“Tumepita wilaya mbalimbali, taasisi za Serikali na kuandaa mapendekezo yetu kama kamati, ikiwamo hili la kusitisha miradi yote mipya ya NSSF hadi hapo tutakapopitia ripoti za CAG,” alisema Mchengerwa.

Alisema kamati inataka kujiridhisha kama kiwango cha fedha kilichotengwa katika miradi hiyo kipo sahihi.

Mchengerwa alisema baadhi ya miradi waliyoitembelea ni pamoja na ujenzi wa nyumba eneo la Kijichi na daraja la Kigamboni.

Alisema kamati imetoa maelekezo kwa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Mifuko ya Jamii (SSRA) kuangalia miradi inayoanzishwa na mashirika wanayoyasimamia pamoja na sera ya uwekezaji.

“Ni vyema tukajiridhisha kama mchakato wa uanzishwaji miradi, ushauri wa kitaalamu umekidhi matakwa,” alisema Mchengerwa.

Aliongeza kuwa zipo nyumba nyingi za mradi ambazo hazina wapangaji, hivyo ni vyema ikafanyiwa uchunguzi kama miradi hiyo ilianzishwa kwa ajili ya kupata asilimia kumi.

“Ipo haja ya kupitia mchakato wa miradi hii ili kuona kama sera ilifuatwa,” alisema Mchengerwa.

Alisema wameiomba Serikali iwasilishe mbele ya kamati hiyo ripoti ya CAG kuhusu mashirika hayo ili waweze kutoa mapendekezo kama yana upungufu na hatua za kuchukua.

Wakati huohuo, Mchengerwa alisema wameipa wiki mbili Serikali kuhakikisha inakabidhi taarifa sahihi za ujenzi wa jengo la ofisi ya Makamu wa Rais ambalo kabla kufunguliwa linaonekana limechakaa.

Alisema cha kusikitisha asilimia 98 ya malipo ya jengo hilo tayari yamefanyika, jambo ambalo ni kinyume cha sheria.

Mchengerwa alisema kamati imeagiza CAG afanye ukaguzi ili kubaini fedha zilizotumika kama zinalingana na thamani ya jengo.

Kamati hiyo pia imeitaka SSRA kutatua tatizo la ofisi za kudumu haraka iwezekanavyo, kwani tangu waanze kupanga mwaka 2008 hadi sasa wametumia Sh bilioni 4.5 kulipia pango.

Alisema kila mwaka mamlaka hiyo inatumia Sh milioni 600, hivyo ni jambo jema kuanzia sasa watafute sehemu ya kujenga ofisi ya kudumu.

Chanzo: Mtanzania
 
Hii nchi ina shida ya kutothamini shughuli za taasisi, kujenga nyumba wangeachiwa NHC tu hii mifuko kama in ataka faida ingekuwa inakopesha fedha kwa makampuni ya kibiashara ili kusiwe na muingiliano wa kujaza majengo ya bei ghali yasiyomnufaisha mtanzania wa kipato cha kati, PPF, NSSF, LAPF PSPF wooote wanajenga nyumba za gharama kubwa atakaa nani wakati wengi kipato chetu ni cha chini?
 
Kuna haja ya kuanza kujifunza hii kitu inaitwa Ujasiriamali manak tunapokwenda ........
 
Wadau nashindwa kuelewa kabisa hizi Kamati za Bunge zinayachunguza nini katika hayo Mashirika ya Umma Na kushindwa kubaini ubadhirifu Mkubwa Na wa kutisha wa hayo Mashirika?Bunge lililopita la Awamu ya 4 kupitia kamati yake liliimwagia SIFA nyingi NSSF wakati kutembelea Miradi yao ya Daraja la Kigamboni,Mradi wa Dege Kigamboni lakini Leo hii Miradi yote hiyo imegubikwa Na UFISADI WA KUTISHA uliopelekea Hata Mkurugenzi Mkuu Bw.Ramadhani Day kuondolewa katika hiyo nafasi.Wakati umefika Kwa Bunge kuteua Wenyeviti wa Kamati wenye sifa (Elimu)Na uwezo Mkubwa kuliko utaratibu wa sasa wa Spika kuteua Wenyeviti atakavyo Na wajumbe wake bila kuzingatia kama wana sifa (Elimu)Na uwezo wa kubaini mambo pia asichague Kwa kujali Itikadi.Madhara ya hayo ndio Leo tunaambiwa NSSF ni JIPU KUBWA.
 
Hii nchi ina shida ya kutothamini shughuli za taasisi, kujenga nyumba wangeachiwa NHC tu hii mifuko kama in ataka faida ingekuwa inakopesha fedha kwa makampuni ya kibiashara ili kusiwe na muingiliano wa kujaza majengo ya bei ghali yasiyomnufaisha mtanzania wa kipato cha kati, PPF, NSSF, LAPF PSPF wooote wanajenga nyumba za gharama kubwa atakaa nani wakati wengi kipato cheyu ni cha chini?

Hiyo ni miradi ya kujitajirisha inayofanywa na wakurugenzi pamoja na bodi zao,kwenye hizo kandarasi ndio kuna ulaji mkubwa wa hela ya wanyonge,kuanzia kufanya tathmini ya mradi,kununua viwanja hadi kujengwa jengo kote ni hela nene,halafu mwishoni hayo majengo huwa makazi ya popo baada ya muda mfupi ,kwa kodi na gharama walizotumia sio rahisi hela kurudi kwani huwa wanaongeza cha juu zaidi kiasi kinachofanya hata kodi ya hayo majumba kuwa aghali sana,pamoja na yote utakuta bado hiyo mifuko ya hifadhi na NHC baado wanazidi kuporomosha hiyo mijengo kuna nini?kwanini hawawekezi kwenye biashara nyingine kama masoko ya hisa hata huko nje,hilo ni tone la maji bado kuna wengine wamekopeshwa na hiyo mifuko japo sio wanachama ,walipoona wanaanzwa kudaiwa wamekuwa wakikimbilia mahakamani,mmojawapo ni Dj mwanasiasa maarufu na kiongozi wa chama cha siasa,nadhani mnamjua.
 
Hiyo ni miradi ya kujitayarisha inayofanywa na wakurugenzi pamoja na bodi zao,kwenye hizo kandarasi ndio kuna ulaji mkubwa wa hela ya wanyonge,kuanzia kufanya tathmini ya mradi,kununua viwanja hadi kujengwa jengo kote ni hela nene,halafu mwishoni hayo majengo huwa makazi ya popo baada ya muda mfupi ,kwa kodi na gharama walizotumia sio rahisi hela kurudi kwani huwa wanaongeza cha juu zaidi kiasi kinachofanya hata kodi ya hayo majumba kuwa aghali sana,pamoja na yote utakuta bado hiyo mifuko ya hifadhi na NHC baado wanazidi kuporomosha hiyo mijengo kuna nini?kwanini hawawekezi kwenye biashara nyingine kama masoko ya hisa hata huko nje,hilo ni tone la maji bado kuna wengine wamekopeshwa na hiyo mifuko japo sio wanachama ,walipoona wanaanzwa kudaiwa wamekuwa wakikimbilia mahakamani,mmojawapo ni Dj mwanasiasa maarufu na kiongozi wa chama cha siasa,nadhani mnamjua.
Na ndio sababu nikasema kujenga nyumba nchini waachiwe NHC peke yao, hii itasaidia kupunguza haya madudu.
 
Walikuwa wanasifia walishapata mgao wao ndiyo maana walisifia sana.
 
haina faida ni sehemu ya wapigaji baadhi ya shughuli zifutwe tuu..wao na nyumba wapi na wapi..Nyumba bei ghali faida kwa wageni waliokatwa mafao Watanzania..
 
Kamati zenyewe za wabunge wala rushwa, hakuna jipya ni kwamba walipewa rushwa wakayafumbia mamcho, awamu hii wameendeleza ulaji wao wakatumbuliwa.
 
Haya sasa ile report ya CAG mliyokuwa mnaishupalia humu ndan jana na juz mliitoa wapi?

Mnachukua report zenu za kufungia maandaz kisha mnaziita CAG report?
 
Wadau nashindwa kuelewa kabisa hizi Kamati za Bunge zinayachunguza nini katika hayo Mashirika ya Umma Na kushindwa kubaini ubadhirifu Mkubwa Na wa kutisha wa hayo Mashirika?Bunge lililopita la Awamu ya 4 kupitia kamati yake liliimwagia SIFA nyingi NSSF wakati kutembelea Miradi yao ya Daraja la Kigamboni,Mradi wa Dege Kigamboni lakini Leo hii Miradi yote hiyo imegubikwa Na UFISADI WA KUTISHA uliopelekea Hata Mkurugenzi Mkuu Bw.Ramadhani Day kuondolewa katika hiyo nafasi.Wakati umefika Kwa Bunge kuteua Wenyeviti wa Kamati wenye sifa (Elimu)Na uwezo Mkubwa kuliko utaratibu wa sasa wa Spika kuteua Wenyeviti atakavyo Na wajumbe wake bila kuzingatia kama wana sifa (Elimu)Na uwezo wa kubaini mambo pia asichague Kwa kujali Itikadi.Madhara ya hayo ndio Leo tunaambiwa NSSF ni JIPU KUBWA.

Tatizo sio sifa na elimu za wabunnge husika bali "Cancer" ya ufisadi iliyolikumba taifa letu! Hulka ya kila anayepata nafasi ya mamlaka ya umma kuichukulia kama fursa ya kujinufaisha binafsi yeye na walio karibunae; makosa kutoadhibiwa na kwa hiyo kujenga utamaduni wa kila mtu kufanya apendavyo na wakubwa wenye dhamana kuyalinda maovu hayo!
 
Mwaka huu! Atabakia nani? Labda makanisa na misikiti tu mashirika ya umma hamna kitu yote hasara kwa taifa
 
Haya sasa ile report ya CAG mliyokuwa mnaishupalia humu ndan jana na juz mliitoa wapi?

Mnachukua report zenu za kufungia maandaz kisha mnaziita CAG report?
Mbona una haraka mkuu ripoti ya CAG imeandaliwa na binadamu na waliotoa taarifa ni binadamu, kujadiliwa Bungeni ni taratibu za kisheria tu mkuu lakini as for now report is out and available
 
Wadau nashindwa kuelewa kabisa hizi Kamati za Bunge zinayachunguza nini katika hayo Mashirika ya Umma Na kushindwa kubaini ubadhirifu Mkubwa Na wa kutisha wa hayo Mashirika?Bunge lililopita la Awamu ya 4 kupitia kamati yake liliimwagia SIFA nyingi NSSF wakati kutembelea Miradi yao ya Daraja la Kigamboni,Mradi wa Dege Kigamboni lakini Leo hii Miradi yote hiyo imegubikwa Na UFISADI WA KUTISHA uliopelekea Hata Mkurugenzi Mkuu Bw.Ramadhani Day kuondolewa katika hiyo nafasi.Wakati umefika Kwa Bunge kuteua Wenyeviti wa Kamati wenye sifa (Elimu)Na uwezo Mkubwa kuliko utaratibu wa sasa wa Spika kuteua Wenyeviti atakavyo Na wajumbe wake bila kuzingatia kama wana sifa (Elimu)Na uwezo wa kubaini mambo pia asichague Kwa kujali Itikadi.Madhara ya hayo ndio Leo tunaambiwa NSSF ni JIPU KUBWA.

Watu wengi waliamini kuwa kamati ya Bunge ya PAC chini ya Zito na Filikunjombe ilikuwa inafanya kazi kubwa lakini kiuhalisia ndiyo haya tunayoyaona leo. Wengi tunajua kuwa Zito ni mzuri sana kwa maneno.

Mimi nadhani wakati kamati hii mpya ya Bunge ya PAC inapotoa maelekezo ya uchunguzi wa NSSF, ingetoa maelekezo pia kwa TAKUKURU iwachunguze wajumbe wote wa Kamati ya Bunge ya PAC iliyopita na M/Kiti wao Zito. Wachunguze ili kuujua ukweli ni kwa nini pamoja na wizi wote uliokuwa unafanyika NSSF chini ya Dr. Dau, PAC chini ya Zito waliendelea kuisifia NSSF na Dr. Dau.
 
Mkuu nimekupata PCCB waichunguze Kamati ya PAC iliyopita Kwa sababu ilipitia Miradi ya NSSF Na kuisifia lakini Leo hii Miradi hiyo hiyo ni UFISADI MKUBWA
 
Back
Top Bottom