NSSF si shamba la bibi tena

Mkuu tunawaona pale Kariakoo siku za Ijumaa wanaswali hadi barabarani, wanazuwia njia.
Mengine kaushia tu yapite.
 
Mwezi Julai 2018 wakati Mifuko ilipokuwa inaunganishwa ukaguzi wa wataalamu waliofunga mahesabu ya PPF walitanabahisha kuwa thamani ya Mfuko wa PPF ilikuwa ni Shilingi trilioni 3.1 wakati shirika la NSSF lilikuwa na thamani ya Shilingi trilioni 3.25.

Ppf kuwa na thamani ya 3.1trilion,
Hizo ndoto za mchan

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hivi huyu Dau ambaye anasifika kwa kuhujumu NSSF ana kinga ya nani asifikishwe mahakamani?
Yani utawala huu wa Magufuli ambao unasifika kwa kusimamia sheria umekwama wapi dhidi ya Dr Dau?
Kama hilo halijafanyika miaka minne sasa, yote mnayosema dhidi yake ni unafiki uliotukuka.
Mahakama ndiyo inayoweza kumtia mtu hatiani na siyo porojo za vijiweni kama hizi.
 
Dau alifanya vitu vikubwa vinavyoonekana pamoja na upigaji wake. Kuna hata tetesi kuwa alisaidia sana fedha za kampeni za Chama Tawala katika siku zake. Hapo nafikiri ndipo anapowabana na wakaona heri wampeleke kule akawe balozi na azibe mdomo wake.
 
Huu uzi una changiwa na wafanyakazi wa NSSF na PPF, ni vita ya team Erio na Team NSSF wazawa.

Anyways.

Kila mtu ashinde mechi zake!
 
Kama ndiyo hivyo hakupiga ila mamlaka zake za uteuzi zilikuwa zinajua alichokua anafanya.
Dau alifanya vitu vikubwa vinavyoonekana pamoja na upigaji wake. Kuna hata tetesi kuwa alisaidia sana fedha za kampeni za Chama Tawala katika siku zake. Hapo nafikiri ndipo anapowabana na wakaona heri wampeleke kule akawe balozi na azibe mdomo wake.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Uelewa wako ni finyu...soma tena kwa utulivu nilichokiandika.
Acha mhemko.
Hakuna cha maana ulichoandika na wala hukujibu hoja yangu ya msingi kwamba Erio yuko kwenye madaraka hayo ya MD kuanzia enzi za PPF kwa kuwa Godfather wake ni mjomba wake Mkapa na siyo CV yake au performance whatsoever!!
 
Na watu watakuja sana kuponda ila all in all nssf ilifikia pabaya...uwekezaji mwingi ulikua wa kupiga na udini ulitamalaki....hoja hubishwa na hoja...kama mnapingana naye leteni hoja hapa sio porojo ..wacha magu atunyoshe tu
Nafuu NSSF ile kuliko hii unayoifagilia. Kuhusu upigaji unaodhania ulikuwapo ni fikra mbovu juu ya miradi kama wa Daraja la Kigamboni. Kama unaidharau NSSF iliyo finance kwa mfumo wa Build, Operate and Transfer daraja la Kigamboni basi na wewe ni mlemavu wa ubongo.
 
Mzee we tetea kibarua....kuna wadau nawajua maboss wako wanakwambia daraja ndo mradi pekee ulioleta faida kwengine kwote chenga unadhan kwanini rais alisimamisha ujenzi kigamboni na toangoma....halafu mlikua mkifuatiliwa mnaweka hongo kama mlivyomkopesha mabilion zito ya lekatukidite sijui
 
Kiukweli hata mimi nakuunga mkono bwana ulio! Nssf ya Dr Dau jamani ilikuwa km unadai 3ml. Lazima uache laki laki zakutosha vinginevyo hutapata check.. ndg URIO WE KAZA BUTI ila hao mameneja wa mikoani uliowaacha waliokuwa wa nssf waangalie sana kama cyo wao basj wawaangalie watendaji wao maana mikoani ndio shida! Ulio komaa na mungu akusimamie.
 
Kuna shida hiko NSSF naona team Erio mmejibu mapigo ! Ila jamaa toka aingie NSSF shavu linakuja ...
 
suala la korido kugeuzwa misikiti wala sishangai. inaweza kuwa kweli. ukienda ofisi za The Joint Finance Commission utayakuta sana mambo haya ya kuswali ofisini. ndugu zangu waislam badilikeni.
Kwako wewe kuswali kubaya ni kule mtu akisujudu na kusimama wima kwa utulivu ila mtu akifumba macho na kujigusa usoni mabegani akiwa anakula mbele za watu na ofisini kwake ni sawa tu..
Kuna tatizo gani mtu anaposwali ofisini kwake kama haadhiri kazi yake?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
kuswalia ofisi ya umma ndiyo wema?

Ukienda kwenye mgahawa kabla ya kula hubsali weye wakristo mbona mna nongwa?? Muislam anaswali mara tani kwa siku na popote pale yeye anaweza kufanya ibada sio lazima ndani ya msikitii
 
Katika makala hii ningeona majibu ya wastaafu na staiki zao basi ningeweka umaskini.
Pia wateja wengi wa NSSF ni watumishi wa Serikali ambao wengi wao ni wa kipato cha chini.
Ila lengo la uzi huu ni nini? Kumfagilia Urio au kumnominate Dau km Muislam wa Kwanza ktk List ya Mafisadi Sugu wa Tanzania?
 
Relax atumbui nssf karibuni
 
Nssf wanaboa kitu kimoja tu hii issue ya 33.3% yao. Yaani hawakupi hela yako yote wanakupa kidogo kidogo tena for 6 months.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…