Mimi kama mdau na mnufaika wa mafao napata changamoto.
Niliacha kazi na nikaandika barua kwamba nakwenda kujiendeleza na masomo nikitegemea kutumia mafao yangu katika elimu kama kujilipia ada na kadhalika nafika nssf nauliza utaratibu naambiwa wewe huwezi kupata nssf hadi ufikishe miaka 55.
Kulingana na huu utaratibu nimelazimika kuacha kujiendeleza kielimu na kurudi mtaani angali pia sina kazi wala biashara.
Ndugu zangu kuna maswali kadhaa yananijia kichwani
1. Je ninauhakika gani kama nitafika miaka hiyo kwa hali ninayopitia wakati huu
2. Je, taasisi hii imewahi kufanya uchunguzi wowote juu ya changamoto wanazopitia wafanyakazi ambazo zinawafanya kuacha kazi?
3. Je, mafao hayo yanauhusiano gani na elimu na miaka 55?
Nadhani tusibaki kushikilia jambo hili la miaka 55 maana ni uonevu na unyanyasaji raia wanapitia changamoto nyingi mtaani na wanajua fika kwamba wana pesa sehemu.