Ta Muganyizi
R I P
- Oct 19, 2010
- 5,355
- 2,737
Wapo Watanzania wengi kwenye sekta binafsi wanaofanya kazi kwa muda mfupi ambao hawakujaaliwa kupata ajiria za muda mrefu serikalini au mashirika ya umma.
Wanapomaliza mikataba yao au mazingira ya kazi kuwa magumu huamua kurudi nyumbani huku wakitegemea kibubu chao (NSSF) kuwa msaada wa kuwasaidia kusongesha maisha. Cha ajabu kibubu chako mwenyewe kinakugomea na kukuwekea masharti kibao kuhusu hela yako.
Sasa kwa hali halisi.....baadhi ya watu walioko kwenye mfuko huo wanajiuliza, mbona kiingiacho kutoka kinakuwa shida. Zinanyonywa na nini hela za wanachama? Kama kweli hela zipo kwa nini aliyeziweka asizipate?
Ni sawa na kuweka kibubu chini ya kitanda ukawa unatupia miambili miambili, ila siku unazihitaji unapewa masharti kibao eti mara mpaka uzeeke, mara nini sijui.
Kama hela iliyowekwa imo kweli fanyeni utaratibu muwape wenyewe. Sio muwanyonye damu hata kwa kidogo walichochangia. Picha inayokuja haraka ni kuwa hela imeliwa na kibubu!!!!! Haipo. Kama ipo wapeni wenyewe.