Ninashangazwa sana na mambo ninayoyaona NSSF. Kila mara wanaringia miradi mikubwa na miundo mbinu ya majengo wanayojenga kwa kutumia fedha za wanachama bila kuzingatia maendeleo hayo yanawasaidiaje wanachama ambao haswa ndio wadau na walengwa wakubwa wa mfuko huo. Ukiwauliza wanasema sheria ya mifuko ya hifadhi ya jamii inawabana utadhani mifuko hiyo ni "imani" na sheria hizo ni "Biblia".
Ninaomba wafanyakazi wote wanaopeleka michango yao NSSF waungane na kudai ubora wa huduma.
1. Mafao wanayolipwa baada ya kutoka kazini yaongezewe riba!. HIzo riba NSSF inapokea kwa ujenzi wa miradi na sasa nasikia viwanda, itoe faida pia kwa wenye fedha ambao ni wadau.
2. Kama vile NSSF inatoa mikopo kwa wakubwa na serikali, ITOE MIKOPO YA NYUMBA KWA WANACHAMA WAKE ILI WAJIWEKEE MAISHA BAAADA YA KUSTAAFU NA si kusubirisha mafao ya kustaffu wakati wamekuwa wazee hawawezi hata kuhimili misuko suko na hata sifa ya kukopa benk wanakuwa hawana, na benki zinatoa mikopo kwa gharama kubwa. Mikopo itolewe kwa utaratibu wa mtu mmoja mmoja ajili ya nyumba ama ardhi na malipo ya mikopo hiyo yajumulishwe na michango ya mwezi. Hati za nyumba na viwanja zibaki NSSF hadi mkopo unaisha kulipwa. Huo ndio ustawi wa wastaafu.
NSSf ukiwauliza wanakuambia eti wanakopesha saccos bila hata kujua mikopo ya saccos ilivyo na gharama kubwa na haina tija kwa zaidi ya siasa na ama mtu awe na dharura ambayo inahitaji fedha bila kuangalia gharama. Utajega nyumba kwa mikopo hiyo? Kwamba ili ukope let say 100,000,000/= sharti uwe na akiba ya 50,000,000/=, halafu unalipa riba ya 100,000,000/= na riba ni kubwa zaidi hata ya mabenk? Ninaomba iweni serious na maisha ya wateja wenu.
Pengine NSSF inaweza kufurahia wastaafu kufariki mapema ili kuondokana na malipo ya mafao lakini kuna thawabu kubwa kuokoa maisha ya mtu bila malipo kuliko adhabu iliyoko katika kushangilia mauti ya mtu kwa fedha.
Kama NSSF hakuna wataalamu wa ubunifu na uratibu wa huduma za mikopo, nendeni kwenye watoa mikopo waliobobea na wabunifu kwenye hizi huduma kama PRIDE, CRDB n.k wawatengenezee kitu ambacho pia kitawafanya mpate wanachama wengi wengine bila shurti na hivyo kuongeza mapato. Ninajua kabisa hamna wataalam na mnaweza kuona hii itawapa shida lakini ni raishi sana kwenu kumanage mikopo kuliko hata hayo mabenki.
Kama sheria hairuhusu, pelekeni mswada wa marekebisho ili wanachama wenu wanufaike na pia muimarishe mizizi yenu kwenye industry.
KUENDELEA KUJIVUNIA MADARAJA, MAJENGO, MANINI NINI SIJUI NA SASA MARA VIWANDA HUKU WAVUJA JASHO WAKIFARIKI MUDA MFUPI BAADA YA KUSTAAFU KWA AJLI YA MAWAZO NA KUKOSA MAKAZI WAKATI MNAUWEZO WA KUBORESHA MAISHA YAO TENA KWA FAIDA, NI UKOSEFU WA MAONO NA NIA NJEMA.
Mwisho wadau wote naomba tuendee kuchangia hapa ili kuwapa mwanga hawa jamaa ili wawaangalie wadau wao kwa jicho la kwanza halafu sifa baadaye.