Noah inauzwa

benitoc

Member
Nov 16, 2010
48
15
Toyota noah inauzwa faster kwa shilingi 7.5 milioni.
contact 0785670038
IMG-20160407-WA0009.jpg
 
Mkuu benitoc,weka details za gari hapa,ili nikikupigia nisipoteze resources zangu kwa mambo ambayo sio siri.
Naamini hii itakusaidia gari inunuliwe FASTER.
Maelezo yapi ya ziada unahitaji? Gari nimeionyesha kwa picha ili ionekane.
 
Hahaha!! Me sio mtaalamu wa magar lakini najua lazima vitu muhimu kama milleage, model, engine capacity, transmission, plate number na record yake ya ajali....nawaza kwa sauti tu.
 
Maswali yote yanajibiwa kwa picha ndugu. Gari sio sawa na nyumba. Gari inajieleza kwa kuiona tu kwani inakuwa na standard specifications. Kama huna uzoefu ni vema ukampata mjuzi au mtaalam wa magari akushauri. Mimi kama muuzaji sitokuwa mshauri mzuri kwako kwani lengo langu ni kuuza sio kutoa elimu
 
Maswali yote yanajibiwa kwa picha ndugu. Gari sio sawa na nyumba. Gari inajieleza kwa kuiona tu kwani inakuwa na standard specifications. Kama huna uzoefu ni vema ukampata mjuzi au mtaalam wa magari akushari. Mimi kama muuzaji sitokuwa mshauri mzuri kwako kwani lengo langu ni kuuza sio kutoa elimu

Acha ubishi wewe, kwa picha gani ulizoweka ili mtu ajue hali ya gari? Picha zenyewe umeficha ficha kama umepiga papuchi, alafu unaambiwa unajifanya mjuaji, hivi wewe ulivyonunua japani ndio uliliona tangazo liko kama huo uharo wako hapo juu?
 
Maswali yote yanajibiwa kwa picha ndugu. Gari sio sawa na nyumba. Gari inajieleza kwa kuiona tu kwani inakuwa na standard specifications. Kama huna uzoefu ni vema ukampata mjuzi au mtaalam wa magari akushauri. Mimi kama muuzaji sitokuwa mshauri mzuri kwako kwani lengo langu ni kuuza sio kutoa elimu
Itakuwa gari ya wizi maana juzi wale jamaa wa bunju walikuwa na noah kama tatu wamepora watu. Unachoogopa kuweka detail za gari ni nini??
 
Tuwe wastaarabu. Kusema ni gari ya wizi wakati imewekwa hadharani si sawa. Kama ni ya wizi nenda polisi. Kama una maelezo ya ziada unayohitaji ni vema ukauliza. Hii ni biashara sio siasa tulete malumbano. Wengine hatuko huko ndugu. Si lazima kila post ujibu unaweza ukakaa kimya
 
Dashboard mkuu ya mhimu sana. Weka picha yake maana naona huna details za gari.
 
Acha ubishi wewe, kwa picha gani ulizoweka ili mtu ajue hali ya gari? Picha zenyewe umeficha ficha kama umepiga papuchi, alafu unaambiwa unajifanya mjuaji, hivi wewe ulivyonunua japani ndio uliliona tangazo liko kama huo uharo wako hapo juu?
kabisa mdau gari kwa kuweka picha tu bila specification details za hiyo gari kweli TZ bado sana aise hizi biashara tunakurupuka kufanya bila ujuzi wowote
 
Tuwe wastaarabu. Kusema ni gari ya wizi wakati imewekwa hadharani si sawa. Kama ni ya wizi nenda polisi. Kama una maelezo ya ziada unayohitaji ni vema ukauliza. Hii ni biashara sio siasa tulete malumbano. Wengine hatuko huko ndugu. Si lazima kila post ujibu unaweza ukakaa kimya
sasa unaogopa nn kuweka maelezo muhimu yanayo husu hiyo gari unataka kuuza gari au umeweka kama urembo mbona hatukuelewi mdau aise
 
Tuwe wastaarabu. Kusema ni gari ya wizi wakati imewekwa hadharani si sawa. Kama ni ya wizi nenda polisi. Kama una maelezo ya ziada unayohitaji ni vema ukauliza. Hii ni biashara sio siasa tulete malumbano. Wengine hatuko huko ndugu. Si lazima kila post ujibu unaweza ukakaa kimya
Kama ni Dalali na Picha ulizopewa ni hizo tu ni bora ukatujulisha.Gari haiuzwi kama unavyofanya wewe.Toa specification zote ili kutupunguzia usumbufu wa kukutafuta kwa gari isiyokidhi viwango.
 
Jamaa anauza bodi (housing ya gari) nyie mmekomaa na mileage, sijui nini na nini!

Nani aliwwambia bodi ina mileage?
 
Maelezo yapi ya ziada unahitaji? Gari nimeionyesha kwa picha ili ionekane.
Mkuu hiyo lugha ya biashara, gari ya kuuza unapiga picha pande zote nje na ndani nadetails zote za gari mfano model, pamoja na maswala ushuru yakoje.
Kuna wengine ni wageni wa magari ili waulize mafundi, madereva au marafiki
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom