kamanda wa mara
Member
- Oct 9, 2017
- 23
- 48
NI MAWAZO TU KWA MFANO
Ukimchukua mtu ukamfundisha kwa muda wa miezi 12 tu mambo muhimu kuhusu mafanikio kama vile kufanya kazi kwa bidii, kuwa mkweli, kuwa mwaminifu, kutofuja pesa, kuwa na malengo, kuwa na ndoto kubwa, kutokata tamaa nk. Mambo ya aina hiyo tu kila siku unamfundisha bila kumpa likizo kwa miezi 12. Halafu baada ya miezi hiyo 12 ya mafunzo hayo ukamwambia aende akatafute maisha. Ni rahisi zaidi kwake kufanikiwa sana kuliko mtu ambaye utamfundisha kwa miaka 17 kuhusu: aina za mawingu, aina na miamba, kwa nini jiwe likirushwa juu linarudi chini, aina za viumbe hai, jinsi ya kuchora bunsen burner au jinsi ya kuiwasha na kuizima na kuisafisha, historia ya biashara ya utumwa, aina za katiba, mchoro wa kupatwa kwa jua, aina za sentensi nk nk.
Kwa wenzangu ambao tumetumia miaka 17 toka chekechea hadi Chuo Kikuu tukifundishwa aina za sentensi au kwa nini meli inaelea na shilingi kuzama tusibaki na hiyo elimu tu tunapaswa kuongeza na hiyo ya kuwa na malengo, kufanya kazi kwa bidii, kutokata tamaa, kuwaza mambo makubwa, kuwa na marafiki sahihi, kujenga tabia ya kutotumia hela yote tunayopata, nk.
Bakhressa hajafanikiwa kwa sababu ya kujua aina za sentensi au "Active Voice" na "Passive Poice".
Hata Dewji amesoma mpaka Georgetown University huko Washington D.C lakini hajafikisha utajiri wa dola BILIONI moja sababu ya kujua aina za mawingu au kanuni ya Archemedes bali alijifunza vitu vya ziada kama kutengeneza connections za watu muhimu maishani, kusoma vitabu, kujali wateja, kufanya kazi kwa bidii nk.
Ameanza kucheza golf huko Florida Marekani mwaka 1992. Kwenye Golf Academy hujifunzi tu kucheza mpira bali kukutana na watu muhimu, kuwauliza maswali muhimu nk..maana mchezo wa golf uchezaji wake unaruhusu hilo kufanyika tena in privacy. Pengine ndo maana baba yake hakumwandikisha Soccer Academy bali Golf Academy.
Sidhani kama unaweza kumcheka Diamond Platnumz kwamba hajui Simultaneous Equation au hajui kuwasha bunsen burner kama wewe. Hahutaji kujua kuwasha bunsen burner ili kufanikiwa maishani.
Wewe unajua kuwasha bunsen burner??
Basi weekend njema
msalimieni venture culture William akisoma hii lazima anitafute
tukutane ramogi kwenye EPL

msalimieni venture culture William akisoma hii lazima anitafutetukutane ramogi kwenye EPL