Prince Nadheem
JF-Expert Member
- Feb 25, 2012
- 1,265
- 1,092
Habari za leo wanaJF. Leo nimekuja na hii hoja juu ya hii ilokuwa ikidhaniwa ni benki ya walala hoi baada ya uwepo wa benki nyingi sana za walala hai ambazo kiufupi wengi wa wananchi hawana maslahi nazo kuanzia huduma hadi accesibility.
Benki nyingi zipo kweye miji mikubwa na majiji, na chache kwenye halmashauri za pembezoni mwa miji mikubwa. lakini kwa wakati wote huo benki ya NMB ipo kwenye karibia halmashauri zoote hapa nchini na imekuwa ni benki tegemeo kwa wafanyakazi wa serikali pamoja na watu wa sekta binafsi kwa kiasi kikubwa kwa huduma mbalimbali za kibenki ikiwa ni pamoja na mikopo ya aina mbali mbali.
Ni kutokana na uwezo mkubwa wa kuhudumia wananchi walo wengi wa Benki hii, serikali ikaamua kupitishia cheki za mishahara kwenye benki hii. Kwa kweli kila kitu kilikuwa sawa na ilikuwa ni maamuzi muafaka kabisa kwa serikali yetu.
Ila mwanzoni mwa mwaka huu (kama sikosei) serikali iliamua kutangza zabuni upya kuhusu tenda ya kusambaza mishahara. kwa kweli ilikuwa ni kitu cha kushangaza maana hakuna benki ingine yenye uwezo mkubwa kama NMB kwa kuhudumia wananchi na hata huduma zao zinaridhisha ukiacha kasoro ndogo ndogo.
Hapo ndipo CRDB akaibuka kidedea. kumbuka ya kuwa crdb hawajafika halmashauri zote hapa nchini. hivyo inakuwa ni pigo kwa baadhi ya wafanyakazi wa serikali.
Sasa kilichotokea ni kuwa benki ya NMB wamesimamisha kutoa mikopo kwa wafanyakazi wa serikali bila kuwa na maelezo yeyote yale...(it is obvious kuwa kwa vile cheque za mishahara hazipitii kwao so wanakinyongo)ila wanasema nendeni CRDB.
ukienda CRDB utaambiwa kuwa inabidi uhamishe account, mshahara uwe unapitia kwao. Hapo ni kwa wale walo katika miji CRDB wanapatikana. kwa maana hiyo wale wa miji midogo kama KIsarawe, Mbinga na miji kama hiyo ni kuwa wamezama.
sasa uamuzi huu unakuwa na implication gani kwa baadhi ya watu? watu watakosa huduma za mikopo ambayo ingewawezesha kufanya uwekezaji kama kufungua/kukuza biashara, kukamilisha ujenzi na vitu kama hivyo (hapo nazungumzia waajiriwa ambao wengi wao marejesho ni kwa njia ya makato ya mishahara yao na dhamana zao ni hiyo hiyo mishahara)
je kwa kufanya hivi serikali imezingatia vigezo gani kuipa CRDB zabuni?
je hii jeuri wanayofanya NMB ndio kuwakomoa wananchi wa kipato cha chini ambao wanategemea zaidi mikopo?
je CRDB kulazimishia mtu ahamishie account ya mishahara kwao hawaoni kuwa wanaleta usumbufu kwa wateja wao wakati inawezekana kuandaa mechanism ya kukusanya marejesho bila ya kuwalazimisha watu kuhamisha mishahara?
Nini hatima ya sie walala hoi kwenye suala zima la kufikia maendeleo hasa ukizingatia na pato letu dogo?
karibuni tujadili na kuelimishana zaidi juu ya hili.