NMB mobile haina msaada kama umekwama

Umenena
 
Sasa kuwahi kupokea mishahara ndo ujanja
 
NMB app ipo..labda wewe tu ndo hujui.
 
hapana mzee unakosea kiongozi sio namba iliyosajiliwa na simu mkononi ndio iwe na bando hapana narudia hapana narudia hapana , wanataka namba iliyosajiliwa simu mkononi iwe kwenye simu tena laini one bando haijalishi hata ukiunga wifi au laini ya pili ikiwa na bando sawa tu mm natumia tigo nmb mkononi bando natumia airtel sema tigo ipo laini one kwaajili ya kupokea code za nmb app internet hata ukiunga wifii haina shida
 
Mimi simu yangu kila nikijaribu inaomba nitumie laini iliyoungwa na nmb, nilishabadili sana laini mzee, mpaka nilishawafata kuuliza. Walichonijibu, weka bando kwenye laini husika
 
Tena nikwambie, unapokuwa umejiunga tayari, hakuna code yoyote inayotumwa labda kama unazungumzia kujisajili na mob app. Kama unaweza kutumia wi-fi why laini ikiwa namba 2 ikatae?
Tumia Simbanking uone maisha yalivyo simple. Hakuna ubaguzi wa namba na app ipo very friendly kwa mtumiaji
 
Kiongozi wewe ni mtumishi wa sector gani? Aliyesema mishara ya watumishi lazima ipite nmb ni nani?
Hebu nenda magereza, polisi kaulize wanapokelea wapi?
Ulipoona lundiko la walimu nmb ndo unasema lazima ipitie nmb. Hujui hata unachokisema.

Mambo yapo hivi, kitambo cheque za mishahara ya watumishi zilikuwa zikipitia nmb. Nmb wakapewa dhamana ya kuprocess kwa maana ya kutuma hizo cheque kwenye mabenki mengine ambako watumishi wanapokelea mishahara.

Nmb wakaanza ukilitimba wa kuwaaminisha watumishi kuwa wao ndio kila kitu. Wakawa wakipewa cheque wanaprocess mishahara ya wateja wao kwanza, huku wamehold mishahara ya watumishi wengine wanaopokelea mabenki mengine. Hii ikawaaminisha watumishi kuwa lazima mishahara ipite nmb.

Sasa basi, kuanzia mwaka jana, serikali iliamua mishahara yote itoke hazina moja kwa moja kwenda kwenye mabenki husika, Kwa maana ya cheque.

Kama unamtu yeyote anaefanya kazi benki au ni ajira mpya muulize hii kitu.

Hope umeelewa. Na nimeandika maana nafaham vizuri sana hii kitu. Foleni zisikubabaishe
 
Ni Msomi wa PhD wa CCM
 
Dah hapa ndio wanapozingua yaani mpaka nitumie line ileile wengine tumeshayachoka baadhi ya makampuni ya simu mfano tigo ni line yao lakini sijawahi iwekea hela kwa sababu ya gharama zao za kipumbavu
 
Nmb
Dah hapa ndio wanapozingua yaani mpaka nitumie line ileile wengine tumeshayachoka baadhi ya makampuni ya simu mfano tigo ni line yao lakini sijawahi iwekea hela kwa sababu ya gharama zao za kipumbavu
Washamba kinoma, ingia crdb ujionee maajabu. Watu wapo vizuri, vijana wengi. Wanazijua product fresh. Nmb wazee wengi, wamechoka kinoma. Mfano nilitaka kupurchase online yani nilizungushwa hiyo siku, mwingine anasema chap chap haiwez mwingine anasema inaweza ikiwezeshwa. Me nikawambia basi iwezesheni.

Wakajaribu weee, mwisho wakasema system inasumbua itabid niibadili hiyo akaunti iwe ya kawaida. Hilo nikalikataa maana ingeanza kuincur makato.

Basi wakanipa option ya kufungua prepaid akaunti tena wanasema ni special kwa manunuzi. Nikakubali. Mchakato ukaanza. Nilipomaliza nikaambiwa niiwekee hela. Nilikuwa nina 90k. Nimeenda kwa cashier akawa haelewi eti, kabla hata hajalogin akasema mtandao wa hiz haupo, eeh bwana ee, niliudhika hiyo siku, nikarudi kwa aliyeifungua akanambia ingia bulk kuna mtu atakusaidia.

Kule nikakuta kuna sister flani nikamuuliza kwann mtandao wa prepaid haupo eti akajifanya kushangaa, akaniuliza nimejuaje. Nikamwambia cashier kasema. Akaichukua kadi yangu na hela akalogin akadeposit ile hela fresh. Akachukua simu akamcall huyo cashier akaanza kumind. Mwisho akamwambia akija mteja wa prepaid mwelekeza aje bulk.

Hii ikanipa picha kabisa kuwa hawa staff ni viazi kwakuwa hawazijui product zao.
 
Sasa kuwahi kupokea mishahara ndo ujanja
Hivi weww uliye benk tofauti na nmb una nn!?? Unautajiri gani !!?? Hizo benk zina unafuuu gani!?? Acha tambo za kishamba huna loloteeee !!!eti nmb benk ya kizeee ya babako ya kijanja ni ipi!??
 
Hata crdb app yao ya sim banking pia inagoma kufunguka ukiwa hauna salio kwa watuamiaji wa tigo,sijajua kwa mitandao mingine
 
Ina maana ukiwa nje ya nchi au ukitumia Wi-fi huwezi kupata huduma kwenye hii app ya nmb mobile?
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…