Nkamia: Wapinzani wana sura mbaya

Babu wa Kambo

JF-Expert Member
May 2, 2016
559
808
Kanuni inayozuia lugha ya kuudhi bungeni ni kiinimacho kwani mbunge wa upinzani akitoa lugha inayokera, mbunge wa CCM ataomba mwongozo kwa Spika na mara akijibiwa atasimama mbunge wa CCM na kutumia lugha hiyo hiyo iliyoombewa mwongozo.

Jana Mbunge wa Chemba, Juma Nkamia (CCM) aliporomosha lugha za kuudhi baada ya kuwaambia wabunge wa upinzani waliokuwa wakishangilia kuwa wanasura mbaya hadi wanatamani kutapika.

Akichangia hotuba ya makadirio na matumizi ya Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi kwa mwaka 2016/17, Nkamia alionyesha kukerwa na hotuba ya upinzani kuhusu wizara hiyo kwenye sehemu iliyozungumzia uchaguzi mkuu wa Oktoba mwaka jana.

Nkamia alisema uchaguzi umepita na mshindi alipatikana ambaye ni CCM na aliufananisha uchaguzi na mpira kwamba unapoisha uwanjani mtu hawezi kulalamika nje.

“Uchaguzi umeisha, leo mtu anasimama hapa anasema ‘ooh tuliibiwa kura’ mlikuwa wapi wakati mnaibiwa kura?”alihoji na kuwataka wapinzani watafute sababu kwa nini walishindwa na si vinginevyo. “Wanajua mchezaji mmoja akiumia katika timu unachukua mwingine kwenye timu ile ile lakini inakuwaje unachukua mchezaji kutoka upinzani? Kwa hiyo niwaombe tu muwe mnatafakari kwanza,” alisema.

Hali hiyo iliibua kelele na minong’ono kutoka kwa wapinzani, jambo ambalo lilimlazimu Naibu Spika, Dk Tulia Ackson kuwataka wabunge huku akiwataja majina watulie ili mbunge huyo amalizie mchango wake.

Nkamia aliendelea, “We nyosha midomo, fanya nini lakini that is the truth (huo ndiyo ukweli).
Utaongea sana na utapiga kelele sana lakini ukweli ndio huo na umekuingia vizuri. Mimi kelele wala hazinisumbui. Mimi nataka niwashauri kama wakati ujao mnataka kuwa chama kizuri anzeni kutafuta wachezaji wenu,” alisema.

“Nyie pigeni kelele lakini ukweli ndio huo, wenye akili wanajua na wapiga kelele wanajua na najua limewaingia vizuri sana.”

Kijembe hiki kiliwalenga Ukawa ambao katika uchaguzi mkuu uliopita walimteua aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowasa. Ukawa walimteua Lowasa baada ya kuitena na kuihama CCM ambapo alipambana na John Magufuli (CCM) aliyeshinda.

Nkamia akionekana kumlenga mbunge fulani ambaye hakumtaja jina alisema, “We piga kelele, kwanza meno yako yameoza.”

Kwa kuzingatia kanuni, lugha hiyo ni ya kuudhi lakini Dk Tulia asisitiza Nkamia amalizie kuchangia ambapo alitoa mfano wa mwandishi wa vitabu Bernard Taper aliyewahi kusema kwamba kuna watu wakiamka asubuhi wakijiangalia kwenye kioo wanatamani kutapika. “Sasa nyie mnaoshangilia humu mna sura mbaya na mnatamani kutapika,” alisema Nkamia.

CHANZO: Mwananchi
 
Kanuni inayozuia lugha ya kuudhi bungeni ni kiinimacho kwani mbunge wa upinzani akitoa lugha inayokera, mbunge wa CCM ataomba mwongozo kwa Spika na mara akijibiwa atasimama mbunge wa CCM na kutumia lugha hiyo hiyo iliyoombewa mwongozo. Jana Mbunge wa Chemba, Juma Nkamia (CCM) aliporomosha lugha za kuudhi baada ya kuwaambia wabunge wa upinzani waliokuwa wakishangilia kuwa wanasura mbaya hadi wanatamani kutapika.

Akichangia hotuba ya makadirio na matumizi ya Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi kwa mwaka 2016/17, Nkamia alionyesha kukerwa na hotuba ya upinzani kuhusu wizara hiyo kwenye sehemu iliyozungumzia uchaguzi mkuu wa Oktoba mwaka jana. Nkamia alisema uchaguzi umepita na mshindi alipatikana ambaye ni CCM na aliufananisha uchaguzi na mpira kwamba unapoisha uwanjani mtu hawezi kulalamika nje.

“Uchaguzi umeisha, leo mtu anasimama hapa anasema ‘ooh tuliibiwa kura’ mlikuwa wapi wakati mnaibiwa kura?”alihoji na kuwataka wapinzani watafute sababu kwa nini walishindwa na si vinginevyo. “Wanajua mchezaji mmoja akiumia katika timu unachukua mwingine kwenye timu ile ile lakini inakuwaje unachukua mchezaji kutoka upinzani? Kwa hiyo niwaombe tu muwe mnatafakari kwanza,” alisema.

Hali hiyo iliibua kelele na minong’ono kutoka kwa wapinzani, jambo ambalo lilimlazimu Naibu Spika, Dk Tulia Ackson kuwataka wabunge huku akiwataja majina watulie ili mbunge huyo amalizie mchango wake. Nkamia aliendelea, “We nyosha midomo, fanya nini lakini that is the truth (huo ndiyo ukweli). Utaongea sana na utapiga kelele sana lakini ukweli ndio huo na umekuingia vizuri. Mimi kelele wala hazinisumbui. Mimi nataka niwashauri kama wakati ujao mnataka kuwa chama kizuri anzeni kutafuta wachezaji wenu,” alisema.

“Nyie pigeni kelele lakini ukweli ndio huo, wenye akili wanajua na wapiga kelele wanajua na najua limewaingia vizuri sana.”
Kijembe hiki kiliwalenga UKAWA ambao katika uchaguzi mkuu uliopita walimteua aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowasa. UKAWA walimteua Lowasa baada ya kuitena na kuihama CCM ambapo alipambana na John Magufuli (CCM) aliyeshinda.

Nkamia akionekana kumlenga mbunge fulani ambaye hakumtaja jina alisema, “We piga kelele, kwanza meno yako yameoza.”

Kwa kuzingatia kanuni, lugha hiyo ni ya kuudhi lakini Dk Tulia asisitiza Nkamia amalizie kuchangia ambapo alitoa mfano wa mwandishi wa vitabu Bernard Taper aliyewahi kusema kwamba kuna watu wakiamka asubuhi wakijiangalia kwenye kioo wanatamani kutapika.

“Sasa nyie mnaoshangilia humu mna sura mbaya na mnatamani kutapika,” alisema Nkamia.
 
Nkamia VOA walikuwa wanakutaka sana ukachukue nafasi ya Jerome danford kazembe,unasauti zuri sana umeniuzi sana kwenda huko,mimi mwanachama wa CCM mwezako ila bado nilipenda sana uendelee pale kina Salimu mbonde walipoachia,umemsaliti sana
 
Mwenye picha ya handsome nkamia aiweke humu

Hahahahaaaaa
Watu wameishiwa hoja wamehamia kwenye sura za watu.
Kazi tunayo wenye sura zinazoogopa vioo.
 
Katika michango ya budget ya mwaka huu mbuge wa CCM aliongea vitu chanya na kweli anaweza kumshauri raisi wake ili Tanzania isonge mbele ni Mh.Bashe pekee wengine wapo katika kuendeleza vita ya kampeni bungeni
 
Huyu jamaa sijui kama huwa yuko sawa...hii si mala ya kwanza kutukana watu....ana lugha inayokera sana....something must be wrong with him.
 
Nimelielewa hili la kukodi wachezaji toka timu pinzani halafu mtegemee kushinda game.... Nadhani hili ndio tusi kubwa zaidi kwa wapinzani kuliko kuambiwa wanasura mbaya.

Amewashauri muanze kuandaa wachezaji wenu mapema, sio siku inafika nusu ya timu yenu wanakua wamekuzwa na wapinzania wenu......halafu mtegemee ushindi.
 
Mtu anaemsikiliza Juma Nkamia ana tatizo! Kwanza ni mtu Wa kujisikia, asiye na elimu ya maana, mtu wa kuijipendekeza ili achaguliwe naibu kama JK alivyofanya! Ana IQ iliyo chini ya kawaida! Ila hili tatizo linaanzia mkoa aliko toka, kibajaji, le mutuz,
haa! eti IQ iko chini ya kawaida! si atakuwa mbuz sasa huyu. umemtusi kisomi aisee. lakin huyu anawaaibisha zaid mke na watoto kuona baba yao anafikiria kwa kiwango hiki kwenye eneo nyeti la kiuongozi. ndo mana hadi leo naamin demokrasia si njia bora ya kuleta maendeleo tangia uwepo wake. ni hatua ya mwisho baada ya kupelekwa kidikteta 'chanya'
 
Hon. J. Nkamia katika ubora wake!!! Speaker please harakisha mashine za kufuatila matumizi ya premium / larger uokoe bunge lako!!!!!!!!!!!!
Sina uhakika kama aliwahi kusoma kitabu cho chote chenye kurasa zaidi ya mia 150.
 
Back
Top Bottom