Kalamu Yangu
JF-Expert Member
- Dec 21, 2016
- 1,099
- 1,042
Niseme sikumpenda,nilimwacha makusudi,
Mwenzangu alinipenda,kwangu alipiga hodi,
Mwishoni nikamtenda,leo yupo na Hemedi,
Bora umepata wako,mpendane mkadumu.
Alinifundisha mengi,alinifunza michezo,
Leo kampata Mangi,pendo liso maelezo,
Kakwepa kuvuta bangi,kuachwa siyo mchezo,
Bora umepata wako,mpendane mkadumu.
Leo nitakwita shemu,si eksi kama kale,
Kuachwa sijelaumu,’singempata yule,
Kwangu tena futa hamu,penzi likalale pale,
Bora umepata wako,mpendane mkadumu.
Sipige simu usiku,mpenzi akulaumu,
Nami nimeshikwa huku,muhibu tanilaumu,
Ukihitaji buku,wangu hadi afahamu,
Bora umepata wako,mpendane mkadumu.
Wala usinichukie,sikupenda nikaacha,
Wa kwako mkumbatie,wala usije muacha,
Wa kwangu msalimie,wewe kwangu ndiwe kocha,
Bora umepata wako,mpendane mkadumu.