Danpol
JF-Expert Member
- Aug 15, 2013
- 5,726
- 8,905
NJIWA UNAYESOMA NIFIKISHIE MAMBO HAYA KUMI.
1. Tafadhali naomba yeyote awaambie Simba hakuna haja ya kuruka ukuta kama mlango upo wazi.
2. Waambie Yanga unapomnyoa mzee hunyoi mvi bali nywele kama zilivyo nyingine.
3. Wataarifu Mtibwa kuwa penda biashara lakini usisahau kula.
4. Wanong'oneze Mbeya City kuwa unahitaji mtandao kutuma barua pepe. Ile sio posta.
5. Waeleze watu wa soka Tanga kuwa Mashua ikipata hitilafu baharini hushuki kusukuma.
6. Wapatie ujumbe wangu TFF kuwa mtoto akipata ndevu hujilinganisha na baba yake na wao hawakumfunda kaka.
7. Msemeshe Waziri wetu wa michezo kuwa waliosinzia msibani hawakuwa ndugu wa marehemu.
8. Paza sauti kwa Ibrahim Ajib na Ndemla kuwa Mwanakondoo aliyebarikiwa kaandikwa kwenye biblia peke yake. Wengine hawana akili ya kuruka hata shimo.
9. Usisahau kuvusha ujumbe huu kwa vilabu vya kanda ya ziwa kuwa kipofu akiona basi ujue jua limezama.
10. Usipoeleweka kote wajulishe kuwa Nicasius Nicholaus Agwanda ( Coutinho Suso ) ubongo wake upo Mwananchi kwenye Gozi la ng'ombe. Kila jumapili na jumatatu. Hili wote wataelewa.
Ahsanteni.
By Nicasius Nicholaus Agwanda ( Coutinho Suso )