GAZETI
JF-Expert Member
- Feb 24, 2011
- 5,277
- 6,673
Nimekumbuka tukio moja la kusisimua ambalo lilitokea nyumbani kwetu, wakati huo nilikuwa naishi na wazazi wangu. NJIWA aliyefungwa hirizi nyekundu aliingia ndani, ilikuwa taharuki babu kubwa. Kila tulipomfukuza njiwa aligoma kuondoka.
Jioni mzee alirudi akiwa amepiga pombe zake. akaamrisha milango na madirisha vifungwe, njiwa akakamatwa kisha akachinjwa, ile hirizi akaichoma moto njiwa akabanikwa akamla mwenyewe maana kila mmoja aligoma.
Miaka imepita, baba amestaafu na hata pombe ameacha. SWALI kwa Gudume na Mshana, matukio haya huwa yanamaanisha nini? Ni zipi hatua za kuchukua yakikutokea?