The Consult
JF-Expert Member
- Jan 20, 2017
- 220
- 252

Kiuhalisia mawazo ya mradi/biashara yapo mengi sana na huwezi kutekeleza kila wazo ambalo umelipata ima kwa njia fikirishi (brainstorming) au njia nyingine, hii hutokana na ufinyu wa rasilimali (scarcity of resources) ukilinganisha na mahitaji yaliyopo.
Hivyo timu ya mradi (project team) inapaswa kuorodhesha mawazo yote ya mradi/biashara na kisha kuanza kufanyia uchambuzi (analysis) ili kujua ni wazo lipi linafaa na lenye thamani kiutekelezaji (worthing project/business idea)
Vigezo vya awali kabisa vya kuzingatia katika uchambuzi wa mawazo ya mradi/biashara yako ni;
- Kiwango cha bajeti (budget constraint), hapa utaangalia kiasi cha pesa kilichopo, kwa ulinganisho na kiasi kinachohitajika kwa ajili ya utekelezaji wa wazo la mradi/biashara husika.
- Urandano na mpango mkakati wa taasisi/kampuni (Strategic plan alignmet), hapa utaangalia ni kwa kiasi gani wazo husika la mradi linaendana na mpango mkakati wa taasisi yako/kampuni yako.
- Upatikanaji wa taaluma/ujuzi stahiki, hapa utaangalia ujuzi unaohitajika ili wazo la mradi/biashara liweze kutekelezeka, na uwepo wa ujuzi/taaluma hiyo katika taasisi/kampuni yako
Katika hatua hii, kuna vigezo vya aina mbili ambavyo hutumika kuchuja mawazo ya mradi/biashara; vigezo vya kifedha (financial criteria) na vigezo visivyozingatia fedha (non-financial criteria).
Vigezo/njia za kifedha katika kuchagua wazo bora la mradi/biashara (financial criteria) kitaalamu hujulikana kama; project financials, financial analysis, business case, au cost/benefit analysis. Njia hizi hujumuisha;
- Net Present Value (NPV), njia hii hukusaidia kujua kiasi cha pesa ambacho mradi wako/biashara yako itakuletea baada ya utekelezaji. (Kwa maana nyingine unaangalia thamani ya fedha ya sasa kwa fedha itakayopatikana wakati ujao, present value of all future cash flows)
- Internal Rate Of Return (IRR); njia hii hukusaidia kuonyesha kwa uharaka upi mradi utarudisha fedha iliyowekezwa (How rapidly will the money returned?)
- Pay back period/time to money; njia hii hukusaidia kuonyesha ni lini/wakati gani mtaji uliowekezwa katika mradi/biashara utarudi kisha uanze kuingiza faida.
- Cash hole; njia hii hukusaidia kujua kipindi katika utekelezaji wa mradi/biashara yako ambapo utakuwa umefanya uwekezaji mkubwa.
The Consult; +255 (0) 719 518 367
Dar es Salaam
Tanzania
Kwa huduma za;
- Uandaaji wa michanganuo ya miradi na mipango mkakati (Project Proposals & Strategic Plans)
- Utoaji wa ushauri na mafunzo (consultancy & trainings) katika maeneo ya Usimamizi wa Miradi na Mipango Mkakati.
Karibu
Your Success is My Desire