More problems
JF-Expert Member
- Mar 26, 2017
- 432
- 257
Kufanikiwa ni ndoto ya kila mwanadamu aweye yeyote yule mwenye utimamu.
Kila mtu katika kazi yake anataka kufika pahala ambapo atajivunia na jamii itatambua uwezo na aliyofanya.
Nimeandika mambo kadhaa ya ambayo hupenda yakakufikisha katika mafanikio unayopenda.
#1. Kufanya kazi kwa bidii na usanifu
Unapofanya shughuli yoyote tumia weledi, ujuzi na akili yako hakika unapata matunda chanya
#2. Jifunze kutokana na makosa kisha songa mbele
Kukosea ni kawaida kwa mwanadamu na tumia makosa yako kufanya vizuri zaidi na kufika unapotaka.
Kumbuka: waliolala pekee ndio hawafanyi makosa.
#3. Fanya kitu unachokipenda
Hii ni mahususi kwa wafanyabiashara. Usifanye biashara ambayo kwako moyoni na akilini hauipendi
Pia Usimuulize mteja nini ufanye badala yake fanya kitu kwanza naye atakapokuja atakuambia hapa ungefanya hivi.
#4. Jifunze kubana matumizi
Tumia kulingana na unavyoingiza na kumbuka kuweka akiba
Jaribu kutumia kanuni mbili zifuatazo
=usipoteze pesa bila sababu ya msingi
=usisahau kanuni ya kwanza
#5. Wekeza
Hili ni jambo muhimu, lakini kabla ya kuwekeza fikiria ni kiasi gani unataka kuwekeza? Utawekeza kiasi hicho namna gani? Thamani ya Mali yako iweje kati ya hazina na thamani
#6. Usiwaamini wanaokukatisha tamaa
Jiamini na amini kuwa unaweza na unalofanya utafanikiwa mradi hujakurupuka. Wanaokukatisha tamaa wawe nguvu ya ww kutenda makubwa
#7. Hifadhi sehemu ya kipato chako kwa ajili ya dharura
Matatizo, shida na mikasa mbalimbali ipo kwa ajili ya mwanadamu, hivyo ni vema sehemu ya kipato chako utenge ili ikusaidie na kukulinda katika dharura kama magonjwa, kufiwa, harusi nk
#8. Mche Mungu
Nimeliweka mwisho kwa kuwa lipo juu ya yote. Naposema mche Mungu sina maana ya kukesha kanisani ama msikitini ukiomba na kuswali.
Bali kutenda yale yaliyo mema tuliyofunzwa na wazazi, walimu na walimwengu tangu utotoni.
Naomba kuwasilisha kwa upendo