Mimi siku za nyuma nilienda salon moja nikanyolewa ndevu kwa manjonjo kibao, mara hiki mara kile...taulo na maji ya vuguvugu nikasafishwa...ni kweli nilitoka pale kidevu kimeng'aa safiiii.
Siku kama mbili au tatu baadae nilianza kupata majibu...kidevu kiliwasha...nikaota mapele mpaka nikakoma. Na ndio ilikuwa jaribio la kwanza baada ya mara zote kuwa natumia mashine.
Basi tangu siku ile sijawahi kupitisha wembe tena kwenye kidevu changu, ni mashine tu hakuna cha ziada chochote kitafanyika, sio mafuta wala sijui after shave au kitambaa cha maji ya vuguvugu.
Na sijapatwa tena na lile tatizo.