Kwa hiyo unamaanisha cuf washike nafasi ya uraisi Zanzibar na bara so! Huo utakuwa UKAWA au CUF
1. Ni ubinafsi kwa CHADEMA kutaka majimbo yote ambayo upinzani una nguvu na wakati huo huo kumtoa mgombea uraisi kwa niaba ya UKAWA.
Katika muungano wowote lazima pawe na kupata na kupoteza. Kuna baadhi ya maeneo muungano utaongeza nguvu zako na kuna baadhi ya maeneo utaku-limit. Hili haliepukiki na ni practice kote duniani. (Hata muungano wetu na Zanzibar ukiuchunguza utaliona hilo dhahiri). Lazima CHADEMA wakubali kupoteza pia.
2. Mgombea Uraisi ndani ya UKAWA
Ni dhahiri kuwa kwa sasa mtihani mzito ndani ya UKAWA ni kumpata Mgombe nafasi ya uraisi....Mgombea ambaye hayupo kushiriki tuu!. Kwa sehemu kubwa ninaamini changamoto hii ni "matokeo ya mapungufu ya kiuongozi ndani ya vyama vya upinzani". Haiingii akilini kuwa ndani ya chama kama CHADEMA, na CUF bado kete pekee ni Dr. Slaa na Mbowe na Prof. Lipumba tuu!.
Tukubali ukweli kuwa viongozi "huibuliwa" na "hukuzwa" na vyama. Kama hatujatoa nafasi kwa vijana na wasomi kuonesha uwezo wao wa kiungozi na uwezo huo ukakua kufikia kujenga ushawishi si ndani ya chama tuu bali kwa jamii nzima, upinzani hautakwepa kuupitia wakati huu mgumu! Matokeo yake kila uchaguzi watakuwa watu walewale tuu hata ambapo uwezo wao wa ushawishi katika jamii umepungua. (Uwezo huu haupo katika utendaji tuu, bali unaweza kupunguzwa kwa vigezo vingine ikiwemo umri)
USHAURI WANGU:
Kutoka na CHADEMA kuwa na nguvu kubwa kwenye jamii (Katika umoja huu)kikubali kubaki kuwa CHAMA chenye wabunge wengi. Na target iwe kuwa na majimbo mengi kuliko CCM. Hiyo itawezekana tuu kwa kupata support ya vyama vinavyounda UKAWA.
Nafasi ya Mgombe uraisi inapaswa kubaki kwa CUF. Changamoto ni kuwa hayupo mgombea ndani ya CUF mwenye ushawishi wa kutosha kumwondoa Magufuli kwa sasa. Professor Lipumba ni mzuri (Tena sana) lakini nachelea kusema kuwa bado hatoshi! Hivyo basi njia pekee ya kuokoa jahazi ni kumchukua Mheshimiwa Edward Lowassa (If at all patakuwa na huo uwezekano) ajiunge CUF na asimame kama mgombea wa uraisi kwa niaba ya UKAWA.
Kumbuka EL anazijua siri nyingi za watakaokuwa wapinzani wake. Mbali ya doa alilonalo (Ambalo linaweza kufifishwa na dhamira yake ya "kuwajibika" na ushawishi mkubwa alionao kwenye jamii) - Tukubali EL anakubalika! Ni mtu sahihi kuiwezesha CUF kushika dola kwa niaba ya wana-UKAWA. Hakuna uwezekano wa CCM kushinda kama utachukua kura za wanaukawa wote plus za CCM wanaom-support EL! Lazima Ukawa watashinda!
Kwa kufanya hivyo Mheshimiwa Lowassa atatekeleza ilani ya CUF kama chama kilichoshika dola lakini pia CHADEMA kama chama chenye idadi kubwa ya wabunge ndani ya Bunge la JMT. Huo ni mgawanyo sahihi wa uongozi. Wakati hilo linafanyika makubaliano yanapaswa kutambua uwepo wa vyama vya NCCR mageuzi na NLD.
Tanzania mpya inawezekana, lakini ni pale tutakapoweka pembeni maslahi ya vyama na kuweka mbelea maslahi ya watanzania!
ANGALIZO: UKAWA ikivunjika litakuwa pigo kubwa kwa vyama vyote vya upinzani na Demokrasia nchini. Kila chama cha upinzani kitashuka ukilinganisha na nafasi kilichopo sasa. Na CCM itakuwa kwa zaidi ya asilimia 25% ukilinganisha na nafasi yake kwa sasa. NIAMININI!
Wewe jamaa ni wa sisiemu na una mpango wa kutuvuruga kisiasa. Si jambo jema na jepesi Lowasa kupeperusha bendela. Kwa kufanya hivyo tutakuwa tuejizika, mtu ambaye mwanzoni tulikuwa hatumkubali sasa atakuwa mtamu kwa lipi na tutawaambia nini watanzania juu ya huyu mtu? Lowasa alikuwa mtamu ccm sisi huku atatuharibia.
Mimi ninamuunga mkono mtoa hoja lakini naomba nikupinge sehemu mbili au moja.
Kwakuwa SISI chadema na CUF ndio tunaonekana kuvutana
Na kwakuwa CUF akipewa akitoa Rais bara akatoa na Zanzibar ni kama Kuiwezesha CUF 100% kuwa ndio CHAMA tawala na wengine watakuwa mapambo tu basi mimi ushauri wangu
MGOMBEA atoke NCCR au NLD
Kwanza tujue kabisa bila kupepesa chini ya Watanzania wanaoangalia mambo juu juu bila uchambuzi wa kina, kwa kiasi fulani uteuzi wa Magufuli umebadili kiasi Upepo huku site/mtaani/uraiani
Hivyo tunahtaji mtu anaeweza toa Upinzani mkali kwa CCM nakuizika kabisa, wazo lako la lowasa naunga mkono, lowasa akija huku, ccm imezikwa milele
Lakn tuondoe uwezekano wa huyo lowasa sisi kama UKAWA lazima tukubali Dr slaa ni mzuri na alikubalika na anakubalika ila hawezi kuwa Chaguo sahihi kum kick out magufuli, nasema hivi kwasababu Dr alipata umaarufu enzi zake bungeni hata alipokuja kugombea uraisi ilikuwa bado yupo hot kwasasa nadhani viatu vile kwa kiasi vimepwaya
Dr pia umri umemtupa, nimesikia mara kadhaa watu hasa wakina mama, na hata leo nimeskia wakisema slaa yule hapana, nadhan mnajua. Katika uchaguzi kuna watu wana deal na mwonekano tu wa mtu kijana/mzee haina ubishi, wengine ile presidential material (mnaoelewa mnanielewa).
Sasa kwasababu hizi ndio naona nafasi ya mtu kama MBATIA, naona nafasi ya mtu kama TUNDU lissu
Hawa wawili wanayofauti sana, lakn kwasasa unaweza jua kuwa mtu kama tundu lissu ukiachia mbali mambo mengine ni gumzo kwa kila mtu ana heat site huku, wengi qanamjua kwasababu ya umaridadi bungeni
Mbatia ana busara, ni mtulivu na presidential material, kwasasa anafahamika kwa kiasi lakn anaweza kuuzwa pia katika kampeni
Nafas tunayo, tusiichezee