Mpendwa umeuliza swali zuri sana tena kwa wakati mwafaka kabla hujachelewa. Kwanza kabisa napenda nikufahamishe kuwa uri na kipato ni sehemu ndogo sana ya kukufanya uowe. Unatakiwa kuoa unapohisi kweli unahitaji mwenza wa maisha na unatakiwa kuwa na TWASWIRA ya mwanamke unayetarajia kuwa naye.
1. Mchumbako kama unampenda kwa dhati kuwa muwazi kwake ukimwambia unapenda nini na ni nini hupendi, mwambie unapenda sana kumuona akiwaje, mfundishe kidogokidogo tena kwa upendo, jipe muda wa matazamio kuona kama kaelewa ama la, kama kaelewa mpongeze na kama hajaelewa baini sababu je ni hataki kuelewa au la.
2. Jiulize kama utakuwa tayari kuvumilia mapungufu yake pasipo kumchoka? uwe wazi juu ya nafsi yako pasipo unafiki ili kuepuka migogoro isiyokuwa ya lazima ndani ya ndoa.
3. Usiowe kwa sababu ya umri, kipato, kwa sababu wenzako wameoa, kwasababu mkeo anafanya kazi ama ni mzuri wa sura bali oa kwa sababu unahitaji mwenza na umempata umpendaye utakaeweza kuishi naye kwa hali iwayo yote.
4. Mchumba wako bado ni binti na anatakiwa kuwa msafi muda wote, unatakiwa ujiulize atakuwaje baada ya kuzaa na baada ya miaka 5, 10, 15 n.k ndani ya ndoa.
5. Kataa suala la mfanyakazi nyumbani kwako ili upime atakavyokuchukulia, kuwa mdadisi na utumie akili ya ziada hasa uulize moyo wako kama unampenda kwa dhati licha ya mapungufu aliyonayo mchumba wako. Ndoa si nyepesi wala si ya kuigiza tena haina warranty. Jiulize, pata majibu kisha chukua hatua.
THINK TWICE WHETHER IT'S TOO GOOD TO LEAVE AND TOO BAD TO STAY OR TOO BAD TO LEAVE AND TOO GOOD TO STAY.