Habari wakuu, ni matumaini yangu mu wazima wa afya. Kwa wale ambao Kwa namna moja ama nyingine hawapo sawa kiafya nawaombea Kwa Mungu awajalie afya tele.
Sasa moja Kwa moja niende kwenye mada, ambapo leo ningependa tujue namna bora ya kutenga classes ambayo ni bora zaidi.
Mfano ukiwa na classes zinazohusiana na User let say ni kama ifuatavyo
1. UserRepository
2. UserAdapter
3. UserItem
4. UserController etc
Na una UI zingine ambazo nazo zitakuwa zina classes zinazorandana na hizo.
Sasa jee ni njia gani bora zaidi ya kuzitenga kwenye package hizo classes kati ya hizi mbili
1.Package kulingana na functions
Hapa unakuwa na package moja ambayo itabeba classes zote ambazo zinafanya the same function mfano kulingana na hizo classes utakuwa na package zifuatazo
1. repository
2. adapter
3. item
4. controller
5. ui
2.Package kulingana na UI
Hapa classes zote zinazohusiana na UI Fulani zitakaa pamoja mfano kulingana na zile class pale juu zote zitakaa package moja ambayo utaiita "user".
Jee kati ya hizo njia mbili ipi ni bora zaidi na Kwa nini iwe hiyo?
Stefano Mtangoo