Njelu Kasaka live ITV

1954tanu

JF-Expert Member
Joined
Jul 19, 2013
Posts
1,038
Reaction score
487
Msikilize aliekuwa kiongozi wa kundi la G55,bwana Njelu Kasaka akiongea katika kipindi cha Dakika 45 kuhusu swala la muundo wa muungano.

Katika kipindi cha Dakika 45 ITV cha leo saa 3 usiku, Mh.Njelu Kisaka akihojiwa juu ya mchakato na mwenendo wa Bunge Maalumu la Katika linaloendelea huko Dodoma ametoa maoni yake huku akionekana kabisa kwamba ni mtu aliyeiva na mwenye kusikiliza hoja kwa makini kabisa. Ameulizwa juu ya mambo mengi mojawapo ni muundo wa muungano.

Akizungumzia kuhusu muundo wa muungano amesema, yeye na wabunge wengine huko nyuma waliunda kundi la G55 kundi lililotetea uwepo wa nchi ya tanganyika. Amedai kwamba, mara baada ya muungano 1964 serikali ya mapinduzi ilianza kudai severignity yake. Taratibu miaka ya 80 Zanzibar ilidai ipewe bendera yake, wimbo wake wa taifa, bandari na gesi na mafuta.

Kwa kupewa hayo, ndipo wao wakaona pia wadai Tanganyika iwe bayana. Amesema Zanzibar wanapodai kuwa kuna kero za muungano, katika 'uhalisia wake' kero za muungano ni mambo ambayo Zanzibar inayadai ili iweze kuwa dola na nchi huru nje ya muungano.

Alipoulizwa kuhusu hotuba ya J.Kikwete katika bunge maalum, amesema hotuba hiyo ilionesha dhahiri kwamba Tanganyika inahitajika na kuwepo na tayari ipo kwani rais kwa kauli yake alisema Zanzibar ijihangaikie kivyakevyake juu uchumi wake na Tanzania bara (Tanganyika) ijishughulikie kivyake kivyake; rais amesema, gesi na mafuta yametolewa kwenye muungano ili wazanzibar wajichimbie na kuyafaidi kivyao vyao hali kadharika dhahabu, gesi na madini ya huku bara ni kwa wabara (watanganyika). Rais alipotamka hivyo, wajumbe wa bunge maalum wakamshangilia sana.Anasema, aliwashangaa wajumbe wa bunge hilo kwani walisahau kwamba Tanganyika ilikabidhi mambo yake yote na uchumi wake kwa serikali ya Muungano. Sasa iweje Zanzibar wao waanze kunyofoa yaliyo yao; na rais kaidhinisha na Tanzania bara (Tanganyika) nao waanze kunyofoa yaliyo yao. Je, hapo kuna muungano!

Akijibu hoja ya serikali tatu, ile serikali ya tatu intakuwa haina nguvu ya kiuchumi na tena inaweza kupinduliwa na wanajeshi wakikosa mishahara ya kulipwa na serikali ya muungano, Mh.Njelu kasaka kasema sio kweli kwamba eti serikali itakuwa haina nguvu za kiuchumi. Amesema serikali zote hazina nguvu za kiuchumi ila zinapata nguvu hizo kupitia bunge linalokuja na mbinu na mikakati ya kutafuta vyanzo vya mapato vya serikali. Hivyo bunge ndilo litakalotafuta vyanzo vya mapato vya seriukali kama ilivyo kwa serikali ya sasa.

Kuhusu jeshi kupindua serikali amesema historia ya mapinduzi ya kijeshi katika Afrika miaka ya 60 hadi 80 inaonesha kuwa kulikuwa na sababu mbali mbali za mapinduzi. Kataja sababu hizo kuwa ni pamoja na; serikali za baada ya uhuru kuendekeza ukabila na ukanda; viongozi wa serikali kujiundia vikundi vya kujilimbikizia mali huku wakiwaacha wanachi wanateseka kwa umasiki; na nyingine ilikuwa ni migogoro ya viongozi wa kisiasa madarakani lakini haikuwa kukosa mishahara kwa wanajeshi. Hizo ndizo sababu za mapinduzi katika nchi za kiafrika.

Juu ya muungano kuvunjika ikiwa patakuwa na muungano wa serikali tatu, mh. Kasaka kasema muungano utavunjika kwa urahisi zaidi kwa muundo wa serikali mbili kuliko ilivyo kwa serikali tatu. Amesema kinachoshikilia muungano hadi sasa ni Zanzibar, wakitaka muungano uvunjike rasmi hata leo utavunjika rasmi. Amesema kwa mfano, Serikali ya Zanzibar ilipotunga katiba yake 2010. Kwa mujibu wa katiba hiyo Zanzibar ni nchi iliyojibainisha na kutaja mipaka yake ya nchi kavu na bahari kama ilivyokuwa kabla haijaungana na Tanganyika. Pia ibara ya 90 ya katiba hiyo inasema katiba ya Zanzibar haitahojiwa na chombo chochote cha JMT.
Hivyo, kama Zanzibar imebainisha mipaka yake ni kwa nini Tanganyika nayo isibainishe mipaka yake?

Amemtetea Jaji Warioba na Tume yake kwamba walichokifanya tume sio kipya na wala sio cha kwao ila ni cha wananchi waliohojiwa na tume hiyo. Pia, amesema kwa maoni yake, hakuona sababu ya rais kutetea msimamo wa chama chake.

Aidha, amesema kama CCM kinajiamini kwamba kina sera nzuri, kina wabunge wengi, kinaungwa mkono na wengi kwa nini kinaogopa kura ya siri? Kura ya siri haina uhuru. Kura nyingi hufanywa kwa siri. Kwa hiyo, CCM wanalo wanaloliogopa.

 
Msikilize aliekuwa kiongozi wa kundi la G55,bwana Njelu Kasaka akiongea katika kipindi cha Dakika 45 kuhusu swala la muundo wa muungano.

Huyu mzee ni wasikunyingi sana aise ningalikua niko huru ningalimsikiliza majukimu yu yamekaba!
 
Msikilize aliekuwa kiongozi wa kundi la G55,bwana Njelu Kasaka akiongea katika kipindi cha Dakika 45 kuhusu swala la muundo wa muungano.

Tanesco imezingua, tuambie anasemaje?
 
CHADEMA WAMTELEKEZA MGOMBEA UBUNGE WAO CHALINZE

Zikiwa zimebakia siku zisizozidi sita wananchi wa Chalinze kupiga kura kuchagua mbunge wao, ni dhahiri kuwa Viongozi wa juu wa Chadema wamemtelekeza mgombea Ubunge kwa tiketi ya Chadema jimboni humo Bw. Mathayo.

Mwananchi mmoja akilalamikia hili anasema, "..tulidhani Chadema ni Chama ya ukombozi, tukadhani maneno ya kuwa kinabagua na kutoa upendeleo kwa wachaga tu ni propaganda za CCM kumbe kweli bwana! Hivi huyu bwana angekuwa mchaga wasingeleta CHOPA hapa?,huku ni kumtelekeza Mathayo kisa sio mchaga!" Alilalamika kijana wa kimasai wa Chalinze mjini.
 

Hicho ndicho alichoongea kwny tv? Au na ww unaleta mada mpya?
 
God bless you mzee kasaka, long live, to see the new reborn tanganyika soon
 
Sijaangalia kipindi, ila kwa nondo hizo, mzee Kasaka anajua aisee!
 
hizi ni porojo tu, rais wa zanzibar na tanganyika wawe na gesi mafuta na dhahabu, rais wa muungano awe na jeshi bila mafuta na gesi siatamtimua mwenzie ili nayeye afaidi ndo jk alikuwa akimaanisha.
 
Sijajua ana umri gani but anafaa kuwa rais wa Tanganyika. Viva Njelu Kasaka (NK).
 
hizi ni porojo tu, rais wa zanzibar na tanganyika wawe na gesi mafuta na dhahabu, rais wa muungano awe na jeshi bila mafuta na gesi siatamtimua mwenzie ili nayeye afaidi ndo jk alikuwa akimaanisha.

Kwani wewe ulishatimuliwa na mmeo ili afaidi unachokijua??
 
God bless you mzee kasaka, long live, to see the new reborn tanganyika soon

Muungano si Ufariki kila Mtu akae kwake , watanganyika wamechoka kuwalea wazanzibar ambao sasa wamejishitukia Kuwa walikuwa wanawaibia watanganyika kwa mda wa Miaka 47 wanataka wafunge mikanda wajitegemee sasa. Ujue Muungano huu ni Kama haupo hv ! Kuna Usanii mwingi Ndio Maana Tume wamekuja na Suluhisho japo Shivji anawabeza baada ya kununuliwa na ccm.
 
East German vs west German waliungana wakawa na serikari moja china na hong kong wana serikari moja kule America kuna serikari moja Obama na makamu wake huku nchi zikiwa na Ma Gavana . Hv kuna Tatizo gani Tanzania Kuwa na serikari moja? Wajaribu moja ikishindikana waje na 3 itasaidia kuikomboa Tanganyika toka kwa Mkoloni Zanzibar .
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…