Nitazipata wapi hizi hadithi/riwaya?

Nitazipata wapi hizi hadithi/riwaya?

mageta

Member
Joined
Aug 26, 2009
Posts
64
Reaction score
33
Habarini wana jamvini?

Nilikuwa msomaji mzuri sana wa majarida ya mwezi kama Bongo, Sani na Tabasamu. Ndani ya haya majarida kulikuwa na riwaya nzuri sana za kusisimua kama MUSAKO WA HAYAWANI, MSAKO WAMR X (riwaya za Eddie Ganzel, na baadae Ray Ganzel ktk jarida la Bongo), DAMU NZITO ya Amri Bawji kwny jarida la Sani. Na hata kwenye jarida la Tabasamu kulikuwa na mtunzi maarufu wa riwayaa ajulikanae kama Emmanuel P. Ndonde alikuwa akitunga hadithiza wapelelezi maarufuakina Micky Reuben na Dick Masamba (kama sijakosea).

Hizo ni baadhi ya hadithi nazozikumbuka, zipo nyingi tu zilizowahi kutungwa na kuchapishwa kwny majarida hayo..kuna baadhi ya hadithi za michoro chini ya wachoraji maarufu kama Fortunatus Ndilla (mtaalam), John Mohamed Kaduma(R.I.P), Aloyce Jacob, Daud Masasi n.k walitunga hadithi za michoro kama, Mlinzi wa zamu, Anga za wenyewe, Hofu ya vizito, hadithi za akina mzee ole, obi, linda n.k. Hiyo ilikuwa ni miaka ya tisini katikati mpaka alfu mbili mwanzoni, magazeti haya yalikuwa maarufu sana. Nilikuwa mdogo kipindi hicho lkn nilikuwa navizia kwa majirani walionunua nami naazima..

Kwa kipindi cha hivi karibun nimekuwa nikipita k'koo kwa wauza vitabu, majarida na magezeti kubahatisha kama wanaweza kuwa na vitabu vya hadithi hizo. Nilibahatisha kupata kimoja tu cha MSAKO WA HAYAWANI..

Je hakuna utaratibu wowote wa kuwashauri watunzi au wamiliki wa hizi hadith wakachapisha kitabu kimoja kila hadithi na kuviuza?..

Maana hadithi hizi zilikuwa nzuri sana na zenye kufundisha.
 
Mie natafuta riwaya moja niliwahi isoma hapa JamiiForums mwaka 2015 mwezi wa Tano.

Ilikuwa ya jamaa mmoja aliyekuwa anasakwa na baba ake auawe. Kama sijasahau jina la mzee wake alikuwa anaitwa mzee kulwa.
Mama yake alikuwa waziri.

Mwenye kuikumbuka naomba anisaidie
 
Mie natafuta riwaya moja niliwahi isoma hapa JamiiForums mwaka 2015 mwezi wa Tano.

Ilikuwa ya jamaa mmoja aliyekuwa anasakwa na baba ake auawe. Kama sijasahau jina la mzee wake alikuwa anaitwa mzee kulwa.
Mama yake alikuwa waziri.

Mwenye kuikumbuka naomba anisaidie
Inaitwaje?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom