Habari wanajamvii ni matumaini yangu mko salama na poleni na kadhia za kila siku,
Niende moja kwa moja kwenye mada, ndugu mimi ni muhitimu wa chuo kikuu Moshi katika ngazi ya ( diploma), nimejitokeza kwenu kuomba msaada wa kazi yeyeto halali itakayonisaidia kujikimu kimaisha.
Historia fupi ya maisha yangu nikua tumezaliwa watano katika familia yetu, nikiwa mtoto wapili katika familia yetu (me) na nilijitahidi sana sana kujikwamua kiuchumi kwa kujishughulisha na biashara ndogondogo za hapa na pale kipindi kiniwa chuo, kikawaida nilikua sichagui kazi ilimradi ilikua halali.
Mnamo mwaka 2017 niliyumba sana katika kupata mahitaji yangu muhimu hali iliyopelekea kuuza simu yangu ya mkononi na kulipa madeni yaliyoniandama kwa vipindi tofauti tofauti, hali ilikua mbaya sana mpaka nahitimu Mungu mkubwa alitokea mtu tu akanifanikisha kueza kulipa baadhi ya madeni niliyokua nadaiwa.
Ila tokea apo nimekua nikijitahidi sana kuomba kazi mbalimbali ndani na nje ya fani yangu, ilimradi mkono uende kinywani, nilifanya kama barman mkoani arusha, na katika kampuni za utalii ila kama office assistant na zote nilikua nalipwa commissions tu. Nilijituma sana katika kazi zote izo na nilidhani itafika kipindi nikaajiriwa kabisa ila nilitolewa njee iliniuma roho sana.
Ila kwa fedha chache nilizopata nikaanza mradi wakufuga kuku kidogo niliona mafanikio ila biashara nayo ilikua ngumu kidogo ukipelekea chakula cha kuku nilikua nakopa faida niliyoipata ilikua inaishilia kwenye kulipa chakula na matibabu kama chanjo za kuku hao.
Nikashindwa kuendelea na biashara hiyo maana mtaji hukueza kuiendeleza biashara yenyewe kabisa hatimaye ikafa. Kwa mda sasa nimekua nikisaka ajira au kazi yoyote ili niweze kujitegemea maana ilinibidi nirudi nyumbani baada yakushindwa kulipia pango nilipokua naishi,
Kwa namna moja au nyingine wadau wote, wanajamii forum nashukuru sana kila mmoja wenu akiguswa kinamna yake atakaye weza niconnect na kazi halali au ajira nipo tayari kuifanya kwa moyo mmoja naamini humu kuna watu wenye tija hata mchango wa mawazo unaeza saidia kwa namna yako yakipekee naombeni nuru iniangazie na mimi nieze kurudi kujitegemea kama apo awali nijikimu mahitaji yangu bila ya wakuomba omba inakera sana ikipelekea mtoto wakiume lazima nipambane.
NB: sijakosea jukwaa najua humu member wengi wapo wanasoma sana jukwaa hili pendwa, mods usihamishe mada hii. Na pia wadau natumia simu ya mtu ila kwa sasa nipo nayo nitajibu kwa kadri ya uwezo wangu, ila pia napatikana kwa 0762468716 kwa mwenye maswali zaidi namna yaku nisaidia..yeyote mwenye msaada wa kazi naombeni natanguliza shukrani zangu za dhati. Mtanisamehe pia kwa uandishi wangu.
Napia napatikana Arusha.
"All the gods, all the heavens, all the hells are within you"