Nitasimama na Rais Magufuli

Duuu nchi kama nani ,yaani tunafanya campaign hivi hivi na COVID-19 ikiwepo.Ili tuone Mbowe kama na wao wanafanya campaign. Haaaa ila Mungu mkubwa ,hapangiwe anapanga
 
Wahi sasa kachukua 35,000 pale Lumumba.
 
Acha umburula wewee wenzako huwa wanapost kwa majina yao ya kweli ili teuzi zisiwapite, nafasi sirikalini bado nyingi tuuu, endelea kumsifia tuu ipo siku na wewe ‘utaonekana’
 
Pamoja na kuwemo ukweli ndani yake ila sifa zimezidi points hivyo kuonekana nia yako ni nini. Tumekuelewa maana duniani hakuna kiongozi mzuri kama Magufuli na wala hapajawahi kutokea na haitatokea. Asante kwa mtazamo wako ila uwe na staha basi kwa kuheshimu pia mitazamo ya wengine wanaopingana nawe usiwaite majina hayo ya kuwadhalilisha maana ni binadamu kama wewe na ni ndugu pia, kwa kufanya hivyo umeondoa hata ile maana nzuri tu uliyotaka kuionesha kwenye uzi wako. Kiongozi mzuri wa watu ni yule anaetambua kuwa anaongoza watu na watu anaowaongoza pia wanamitazamo tofauti tofauti lakini hao wote ni wake hivyo hapaswi kuwapuuza bali kwenda nao na hicho ndio kipimo cha uongozi bora; yaani ni mvumilivu na mnyenyekevu kwa kila mmoja anaemuongoza. Hebu jipe muda kidogo kutafakari je hayo yote yapo pamoja na uliyoyasema hapo juu?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hujui kabisa unachoandika hapa: Tunaye mtu mkabila kuliko mwingine aliyewahi kutokea. Hivi umewahifanya analysis ukaangalia idadi ya mawaziri na manaibu wao wangapi ni wa kabila lake? Umewahi kujua wakuu wa mikoa na wilaya wangapi wanatoka kabila lake pekee? Hivyi unajua chuki aliyonayo kwa baadhi ya makabila nchini? Hivi unajua ni fedha kiasi gani ambazo hazikuwawahi kuidhinishwa na bunge lakini zinafanya miradi kwao huko?

Hivi unafahamu watu wangapi wameuawa, au kupotezwa hadi leo hawaonekani au kuteshwa vibaya mno, rejea akina Lissu, Saanane, nk?

Unajua amejenga mtandao wa kikabila around him unawajua wote wanaomzunguka wanatoka wapi? Hivi unajua kiburi cha bashite kinatoka wapi na bashite anafanya mambo gani kwa nchi hii? Hivi unajua jinsi watu wanavyokosewa haki kwa kufukuzwa bila mchakato na hata baadhi yao kurudishwa pia bila mchakato, unafikiri akili na weledi vinatumia hapo? rejea akina Mwigulu.

Kuna nini cha ajabu kimefanywa miaka 5 iliyopita kuhusu kilimo ambacho ndio sekta inayoajiri 80% ya watz? Hivi unajua makosa yaliyofanyika ATCL na wapi tunaelekea na nani atabeba huo mzigo wa hasara ya fedha za maskini? Wewe umewahi kujua kama ATCL wanapata faida au hasara na umewahi kuambiwa hata siku moja faida au hasara ni kiasi gani?

Hivi unajua mtandao wa watu wake unavyogharimiwa kwa mabilioni ya fedha za maskini? Umewahi kuona ni msafara mkubwa kiasi gani wa watu na magari wanapokuwa wanakwenda chattle?

Labda kama unatumikia ili ufaidike na jiwe bila kujali mamilioni wanaoteseka na uongozi mbovu kabisa.

Tuna kiongozi asiyependa kusikiliza hii inajulikana dunia nzima. Demokrasia yetu imekwenda wapi? Uhuru wa vyombo vya habari tuliokuwa nao upo wapi? Unazungumza usiyoyajua na ni kawaida kwa watz kuwa hivyo ndio maana tunashangawa na kila mtu duniani!

Unaona vile corona inavyofichwa. Unajua ni watu wangapi wameugua na kufa? Kwanini watu wanazikwa usiku? Kwanini visa vyo corona kwa Tz haviripotiwi kila siku kama wanavyofanya Uganda, Kenya, etc? Wewe unaona sawa kujenga uwanja wa ndege wa kimataifa chattle? Hata Dodoma bado hatuna uwanja wa kimataifa! Bado hujui yapo mengi mno.
 
You Neal It!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…