Nitafurahi Benchika akianza na kikosi hiki kesho vs Wydad pale kwa Mkapa

1979Magufuli

JF-Expert Member
Feb 20, 2023
439
1,756
Benchika, nakusalimu na nakupongeza kwa kuibadilisha Simba, kesho ni final mzee wangu, iwe jua au mvua lazima tusimamishe nchi, najua Wydad nao wanachukulia hiyo ni final kwao, watavuruga sana mchezo kwa kulalamika lalamika, kujiangusha kuomba penati na hata kuomba penati.

Sikupangii kikosi najua wewe ni mtaalamu sana hadi umekubalika mapema sana, kama sio wewe Benchika mashabiki tusingeenda uwanjani, makelele ya Ahmed Ally yasingesaidia, sisi mashabiki tulishaamua kukaa pembeni maana kipigo cha mabao 4 kutoka kwa wale wehu kimetupotezea kabisa stimu, hata hiyo kesho tutakuja uwanjani kwa sababu yako Benchika na sio uongozi wala semaji letu, tunakuja kwa sababu umeonyesha mbinu na ufundi kwenye ufundishaji wa Simba.

Benchika, kesho Saido Ntibazonkiza na Sadio Kanoute hawatokuwepo, ushauri wangu kikosi cha kesho chonde chonde Mzamiru Yassin achana naye, mpumzishe kwanza kama kweli unataka kuimaliza mechi mapema.

Nitafurahi ukianza na kikosi hiki kesho.

1 Ayoub Lakred
2.Kapombe
3.Shabalala
4.Inonga
5.Che Malone
6.Abdallah Hamis
7.Kibu Denga
8.Ngoma
9.Chilunda
10.Chama
11.Somba Somba Onana

Mzamiru ana makosa mengi sana, hajui kupiga pasi wala hana nguvu ya kulenga goli, ni ushauri tu mkuu wangu, nakupenda sana Benchika.Kesho tutakuja kukuunga mkono baba yetu.Asante
 
Hivi mashabiki wa Simba mnakumbuka kwamba Wydad kesho anacheza kufa na kupona ili aokote points 3 kwenu?

Game ya kesho ni aibu hapo kwa Mkapa.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom