Nissan xtrail inatumia mafuta kiasi gani kwa uzoefu wako

Nahitaji kununua xtrail 2003 yenye engine ya SR20VET,

Nanunua modeli yenye engine ya SR20 kwa sababu engine hiyo inasifika kwa uimara duniani kote na ni nyepesi kwa mafundi kuirekebisha endapo ikisumbua.

Kwa wale waliowahi kumiliki xtraili hasa ile yenye engine ya 2.0L au cc 2,000 naombeni mnipe uzoefu wenu. Hii gari inakunywaje mafuta ? Binafsi Ningependelea nipate angalau 11km/L au nitembee kilometer 11 kwa kila Lita moja.
SR 20 inatofauti gani na QR 20 kwenye utumiaji mafuta na uendeshaji kwa ujumla?
 
SR 20 inatofauti gani na QR 20 kwenye utumiaji mafuta na uendeshaji kwa ujumla?
SR 20 inaturbo na ina nguvu ya 200kw.
QR 20 haina turbo na ina nguvu ya 103 kw.
Nakushauri utumie gari yenye injini ya QR20.
Ni rahisi zaidi kuitunza kwa muda mrefu na gharama nafuu
 
Mkuu sikiliza nikupe fact kidogo juu ya xtrail as namiliki hili gari huu mwaka wa nne na niliitoa japan, itapendeza kama mtu ambaye hajawahi kumiliki gari za nissan au hata kuendesha gari ya above 1500cc aache ku comment as you have no idea rather mnapotosha.

Kwanza niseme wazi gari za nissan as for Benz BMW range etc hazihitaji mtu mwenye kipato cha mawazo au anayetegemea kuuza baada ya siku chache.This is about purchasingbpower and affordability.

Gari hizi hazihitaji mafundi wa kuunga unga na spea za kufananisha au kufitishia rather genuine spare parts.

Mfano extrail uliyotaja inatumia gear box oil ya fuild matic J ambayo lita moja inauzwa 50,000 ipo kisangani auto ,master cad auto wako msimbazi dar au authorised dealers wa nissan na gari hiyo itahitaji lita 4.

Engine oil inaweza kuwa synthetic au ya kawaida mfano BP standard lita 5 inafika hadi 55,000 ila unatumia lita 4.

Brake.pads mfano zile genuine za mbele ni 220,000.

Hio ni baadhi ya mifano tu ila my point is hizi gari zisizotaka mafundi kanjanja na spea za magumashi.

Juu ya fuel consumption hiyo yako ya 2003 unaweza kwenda hadi 1l/11km with full ac..mimi iko hivyo as ni la.muda na all the time natumia ac hata iwe arusha.

Well,ni gar za kueleweka ila waliozoea vitz starlet etc na ambao wana limited understanding plus kipato cha mawazo watakuambia ni ndoa ya kikristo.

Just ishi ndoto zako as far as you can afford.

Karibu kwenye team ya xtrail!
Mimi naomba kujua agent wa kuuza genuine spare za Nissan mkuu wanapatikana sehemu gani au no yao ya simu kama ipo
 
Mimi naomba kujua agent wa kuuza genuine spare za Nissan mkuu wanapatikana sehemu gani au no yao ya simu kama ipo
Wako wengi ila kama uko dar nenda Mastercad auto msimbazi au kisangani ent..wako msimbazi ila spare za nissan ziko maduka mengi na nyingi ni genuine hatunaga mambo ya kuunga unga.
 
Wako wengi ila kama uko dar nenda Mastercad auto msimbazi au kisangani ent..wako msimbazi ila spare za nissan ziko maduka mengi na nyingi ni genuine hatunaga mambo ya kuunga unga.
Arusha za kuunga sa hivi zinapatikana fresh tu.
 
Mkuu hebu ni connect na fundi mzuri wa hizi gari kama yupo unaemfahamu

Mlioko Mwanza na maeneo ya jirani, leteni gari zenu MORAF GARAGE mtaa wa Rwegasore....

Ni garage ya kisasa yenye mafundi wabobezi hasa pamoja na vifaa vinavyotumia teknolojia ya kisasa....

Ukileta gari yako aina yoyote si tu NISSAN XTRAIL mnayoijadili hapa bali gari "make" yoyote iwe Toyota, Nissan, Hyundai, Mercedes Benz, Peugeot, Isuzu nk nk ikiwa na ubovu wowote kuanzia jumba (body) hadi Engine utapewa masaa ya kusubiri kati ya 6 - 24 kisha unakuja kuchukua gari yako ikiwa kama mpyaaaaa...!!

Ufundi wetu unaanza na kuichunguza gari yako kwa kuiingiza katika chumba maalumu cha kuchunguzia ambacho ni COMPUTERIZED. Stage hii tunaiita "diagnosis stage"

Baada ya hapo tutatambua ubovu wote wa gari yako na mfumo wetu wa computer utakukokotolea na gharama kuanzia vifaa (spares) vinavyopaswa kuwa replaced mfano fuel pump, fan belts, engine oil seals, ball joints nk nk

Baada ya hapo utaulizwa kama unakubaliana na gharama au la. Ukisema, it's okay, basi gari inaingia kwenye chumba cha matibabu (operation room) kutibiwa...

Ukisema, gharama hiyo ni kubwa utalazimika kulipia tu gharama za uchunguzi (diagnosis costs) tu ambazo zina - range kati ya 100,000 - 300,000/= na baada ya hapo unaweza kupeleka gari yako popote kutengenezewa...

Kama utakubaliana na gharama za matengenezo, basi tutakupa masaa kati ya 6 - 24 kusubiri kabla hatujakuita kuja kuchukua gari yako...

Malipo (maintenance fee) hufanyika baada ya matengenezo kukamilika. Hatuchukui fedha advance yoyote kabla ya matengenezo kukamilika...!!

Karibuni sana.

Na muhimu ni kujua ni kuwa HAKUNA GARI YOYOTE AMBAYO NI PASUA KICHWA bali gari aina yoyote kama haipati REGULAR PRESCRIBED ROUTINE MAINTAINANCE na kwa kumtumia fundi mbobezi, basi lazima tu itakupasua kichwa....

Ufundi wa Magari ama vyombo vya moto vyote ni TAALUMA kama zilivyo TAALUMA zingine zote kama udaktari, ualimu, ufundi ujenzi wa nyumba nk nk....

Huwezi kumpeleka mgonjwa wako kutibiwa na daktari mbabaishaji ama kajanja ambaye hakupata training na kuwa certified otherwise utakuwa umempeleka mgonjwa wako kwenda kuandikiwa hati ya kifo...!!

Ndivyo ilivyo hata na kwenye TAALUMA ya motor vehicle mechanics. Ukipeleka gari yako kwa "maafundi nyundo", unahatarisha uhai na efficiency and smooth running ya gari yako.....

Hatuwapigi dongo mafundi wa mitaani, laa. Wapo mafundi wazuri sana, tatizo ni kuwa hawana vifaa vya kazi....

Nawatakia kila la kheri
 
Nipe ABC z hiyo fortuner
Ni Toyota....zamani ilikua zinatokea Toyota Thailand ila kwa sasa ziko za South..Na Uarabuni.Ni zuri kwa muonekano na imara.Ina version nyingi kutokana na miaka...uki google utaona details.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom