JMF
JF-Expert Member
- Jun 29, 2013
- 1,756
- 2,764
Salaam wakuu. Nina options za kuchukua mojawapo ya gari tajwa hapo juu au SUBARU FORESTER baada ya kusumbuana sana na mama watoto kwani tuna gari moja ambayo ndo naitumia kwa shughuli zangu za kwenda kwenye miradi yangu huko kisarawe. Nalazimika kumpeleka kazini ndipo niende kwenye shughuli zangu hivyo hii hali nimeichoka na naona bora nimwachiae Mark II ninunue gari iliyonyanyuka juu kidogo na iliyopo ndani ya bajeti yangu kutokana na adha ya barabara ninazopita kwenye mizunguko yangu. Gari zote hapo juu ni za mwaka 2008 na engine ni cc 2000-2500. Naombeni ushauri kwa mliowahi kuzimiliki, mnaofahamu changamoto zake kama spare, service n.k Asanteni.