Nisaidieni USB Flash Disk Haitambuliwi

Anko Sam

JF-Expert Member
Jun 30, 2010
3,200
820
Nilinunua USB Flash Disk ya GB 8 mwezi uliopita, nimekuwa naitumia kuwekea file za muhimu sana. Leo nimejaribu kuifungua nifanyie kazi mafaili yangu, imeshindwa kufunguka automatically, nimejaribu kutumia njia ya My Computer inaniletea kibox kimeandikwa "Please insert a disk into drive H" kwenye properties inaonyesha capacity "0 bytes".

Nimechanganyikiwa, je wataalamu mnaweza kunisaidiaje kurecover mafile yangu?
 
Swali naona limekuwa gumu kwa wataalamu, hakuna aliye-respond within 24hrs! Au niambieni ni flash disk za brand gani ndiyo hapotezi memory kiurahisi?
 
Itakuwa una flash aina ya KINGSTON DataTraveler 8GB zile ambazo wajanja wanauza mtaani. Kwa ufupi ni kwamba umeshapigwa bao.
 
Je inakuwa detected??angalia hiyo usb haitingishiki??shika mdomo wake tingisha kama inatingishika sana basi yawezekana ina dry joint!
 
Tumia Touchmate au Transcend.

Flash iliyogoma ni aina ya Transend 8GB, situmii aina nyingine, nilishaliwa kwa aina zingine nikakoma kuzinunu. Naiamini sana brand hii lakini safari hii nashangaa! Ni mpya haitikisiki wala nini, je hakuna program ya kufukunyua nitoe file zangu, kama kuna mjanja hapa Dar nimtafute anifanyie makeke!
 
Je inakuwa detected??angalia hiyo usb haitingishiki??shika mdomo wake tingisha kama inatingishika sana basi yawezekana ina dry joint!

Yas, inakuwa detected na massage inakuja "....the USB is ready to use..." lakini nikifungua hakuna kitu inakataa! Nimekwisha jaribu kwenye computer kadhaa lakini wapi! Unanishaurije KakaKiiza?
 
Dah! kurecover flash yenye tatizo kama lako ni ngumu sana mkuu. Ila kama ningekuwa karibu ningekusaidia
 
Jaribu ku run comand ya chkdsk
Vile vile unaweza kujaribu tumia hii tool ya RcoverX ya transcend ku recover files kama itafaya kazi.

MKUU ZING wewe ni NOOMA!, AHSANTE SANA MKUU, imekubali baada ya kutumia hiyo tool. Sasa hebu fanya kitu kimoja, kwa vile nilikuwa nimepoteza matumaini, ni-pm nikurushie TAKRIMA YANGU! THANKS GREAT THINKER!
 
Back
Top Bottom