Nisaidieni hili: Ubakaji wa mwanafunzi wa form six mwenye umri wa miaka 16

TAWA

JF-Expert Member
Jun 23, 2013
3,674
1,572
Nimeona katika taarifa ya habari ya ITV usiku huu kuwa askari mmoja wa jeshi la polisi kikosi cha FFU amefikishwa katika mahakama ya hakimu mkazi jijini Arusha kwa kosa la kumbaka mwanafunzi wa kidato cha sita MWENYE UMRI WA MIAKA KUMU NA SITA.

My take:
Nimejaribu kupiga hesabu zangu naona zinakataa, mwanafunzi wa kidato cha sita kuwa na umri wa miaka kumi na sita labda mwanafunzi huyu kama atakuwa ameanza darasa la kwanza akiwa na miaka mitatu.
Hapa ndipo unapoona weledi wa mahakimu wetu na waendesha mashtaka wetu kuwa upo chini sana.
 
Binafsi niliiona hii nikashindwa hata kushangaa. Hapo wamembambikia msela kesi, hakuna mwanafunzi wa umri huo anayesoma kidato cha sita.
 
Sasa hicho kichaa chake kingempanda huku kashika Smg na ana risasi za kutosha sijui ingekuaje
 
Kosa kama hilo waliwahi kushitakiwa nalo Ribery na Benzema,walishinda kesi kwa kuwa binti huyo aliwadanganya umri na pia alikuwa na umbile kubwa kiasi kwamba huwezi hisi kama ni under 18!
Ila binti wa form 6 kuwa na miaka 16 inatia shaka
 
Huyo askari akate rufaa, asubuhi tu anashinda rufaa yske.
My take:
Ukipiga hesabu ili mtoto mwenye umri wa miaka 16 awe kidato cha sita itabidi awe ameanza chekechea akiwa na miaka miwili, jambo lisilowezekana.

Huyo afande wamemfanyia tu uhuni ama huyo binti ni wa kibosile fulani. Kuwa form 6 kikawaida lazima umri wake uwe zaidi ya miaka 18.
 
Labda binti alirushwa madarasa huko msingi. Nje ya hapo, hakuna form 6 kwa miaka 16.
Kitaalamu mtu anarushwa darasa mara moja tu na si zaidi ya hapo. Hakuna mtu anayerushwa madara mawili kwa wakati mmoja.yaani mtu atoke la kwanza hadi la tatu, hakuna. Hapo huyo askari amtafute mwanasheria mzuri tu, kesi inaisha mchana kweupe.
 
Kitaalamu mtu anarushwa darasa mara moja tu na si zaidi ya hapo. Hakuna mtu anayerushwa madara mawili kwa wakati mmoja.yaani mtu atoke la kwanza hadi la tatu, hakuna. Hapo huyo askari amtafute mwanasheria mzuri tu, kesi inaisha mchana kweupe.
 
Huyo askari akate rufaa, asubuhi tu anashinda rufaa yske.
My take:
Ukipiga hesabu ili mtoto mwenye umri wa miaka 16 awe kidato cha sita itabidi awe ameanza chekechea akiwa na miaka miwili, jambo lisilowezekana.

Huyo afande wamemfanyia tu uhuni ama huyo binti ni wa kibosile fulani. Kuwa form 6 kikawaida lazima umri wake uwe zaidi ya miaka 18.
Huyu bwana kama akikata rufaa lazima ashimde
 
Ndugu,hilo linawezekana,siku hizi elimu ya miaka 4 kidato cha kwanza mpaka cha nne mtu makini anasoma kwa miaka miwili tu na anapiga paper ya form four na anapata credit hivyo anaendelea na Alevel ambayo nayo badala ya miaka miwili anapiga kwa mwaka mmoja anafanya paper ya form six anaingia Chuo!!!nina mifano ya ndugu zangu watatu ambao niliwatoa kijijini baada ya kushindwa kusomeshwa na ndugu huko kijijini nikawaleta Dar nikawaunga QT.Hivi ninavyokwambia mmoja ka-graduate degree ya kwanza UD 2015,hao wawili ndio wameingia mwaka wa tatu November mwaka jana,mmoja yupo UD na mmoja yupo UDOM!!Hivyo acha kukariri kwamba elimu ya sekondari ni miaka 6 kama tulivyosoma sisi,siku hizi mtu serious anatumia three years badala ya six years.
 
Ubakaji ni kosa ata kama huyo binti angekuwa amevuka umri wa kuitwa mtoto; na hili tatizo ni kubwa kwenye jamii kuna watu ambao awaripoti matukio hayo isitoshe kuna shule luluki za boarding huko vijijini tunaambiwa watoto kadhaa wa kike wanapotezewa masomo kisa kupelekewa ndoo za maji tu (wenyewe wanaita mimba za maji) ambapo huko mashuleni kwao kuna uhaba na mabinti inabidi wajisafishe mara kwa mara.

Unategemea waziri wa afya achukue hili swala very serious kwenye kuwalinda watoto ambao wapo kwenye hizi risks na sidhani kama ni swala la mwalimu mkuu tu wa shule given the circumstances kuna hitajika nguvu kazi ya sehemu mbali mbali za jamii kila mtu kupewa majukumu ya kumaliza matatizo kama haya ndio hapo utajua kutokana na changamoto za wizara zingine si kila kiumbe anafaa tu kuziongoza.
 
Back
Top Bottom