I need help
Member
- Nov 14, 2024
- 5
- 5
Habari wakuu, nataka kuleta historia fupi ya Familia yangu ila sipo vizuri kabisa kiuandishi ila mtanivumilia guys sijui hata sehemu ya kuweka aya ni wapi.
Mimi naitwa John (fake name) nimezaliwa katika Familia ya watoto watatu mabinti wawili na wakiume mmoja ambaye ni mimi pia mimi ndio mtoto wa mwisho, nimezaliwa kwenye ukoo wa kichief huko kagera babu yetu alikua na wake watatu hivyo.
Nina baba zangu wakubwa na wadogo plus mashangazi, baba yangu mzazi alibahatika kusoma chuo cha Dar tech miaka hiyo jijini Dar es Salaam akapata kazi huko huko ndipo akakutana na mama wakaanzisha Familia, ninavyosikia baba alikua amejenga huko tandika ila baba alipata taariba bibi yangu anaumwa huko kijijini (mama yake mzazi) baba akaamua kurudi kijijini kumuuguza mama yake ambaye ni bibi yangu mimi, akamuacha mama dar peke yake kwa ahadi atarudi ila miezi mingi ilipita bila baba kurudi kwa Familia yake na ujuavyo miaka hiyo hakuna simu ni kuandikiana barua kwa posta tuu isitoshe mama alikua na mtoto mdogo (Dada yetu mkubwa).
Mama aliamua kufunga safari na kumfata baba kijijini alivyofika alimkuta baba kashaanzasha mahusiano na mwanamke mwingine na wanamtoto ila walikua hawakai pamoja ilitokea vurugu ila walisuruhisha yakaisha na rasmi mama alihamia kijijini jumla wakaanza maisha kwenye nyumba ya babu yetu na ndio akazaliwa Dada ninae mfata na baadae mimi.
Niielezee nyumba ya babu yangu kidogo, kama nilivyotangulia kusema babu yetu alikua chief wa huko alifariki miaka mingi nyuma so nyumba yake ilikua na vitu vingi sana alivyokua anatumia kwenye shughuli zake kama ngoma, Mikuki, visu, ngazi mbali mbali za wanyama na vingine vingi na vyote hivyo vilikua chumbani kwa baba, kama nilivyosema baba alisoma dar tech na alisomea mambo ya welding na dar alikua na ofisi yake nzuri tuu na ilikua inamuingizia kipato kizuri tuu ila alivyorudi kijijini maisha yalikua magumu sana alikua Hana kazi hivyo akaungana na baba yetu mkubwa wakanunua mashine ya kusaga baada ya kuuza baadhi ya maeneo ya babu ili waweze kupata pesa ya kumuhudumia bibi yetu na pesa za kuhudumia Familia zao, ila kipato cha Ile mashine kilikua hakikidhi mahitaji kabisa na isitoshe baba yangu ni mlevi sana so hela yote iliishia kwenye pombe.
Tuliishi maisha ya dhiki sana mama ndio alikua analima mbele ya nyumba ya babu (tulipokua tunaishi) mazao madogo ili tupate chakula, miaka ilisonga Dada mkubwa akamaliza la saba akafaulu akaenda secondary school tukaendelea na maisha ya shida Dada yangu ninaye mfata nae akamaliza la saba akapass pia akaenda secondary nikabaki mimi. Nirudi nyuma kidogo kama nilivyosema tulikua tunakaa kwenye nyumba ya marehemu babu yangu ambae alikua chief mkubwa tuu,Kuna baadhi ya vitu nilikua naviona kwenye nyumba Ile mbali na vitu vya asili nilivyoeleza huko juu ila kulikua na vichuguu vikubwa sana kwenye chumba cha baba yangu (chumba alichokua anatumia babu yangu) tulikua tunavivunja na kusomba ule udongo na kwenda kutupa nje ila kesho yake utakuta vimeota tena kwa kasi ya ajabu tunazoea tena tunaenda kutupa Hilo ni zoezi lililokua linafanyika kila siku na miaka yote.
Toka nakua nilikua nasikia story tuu za mababu zetu jinsi walivyokua wanashindana kiuchawi na kinguvu lakini sikuwahi kupelekwa wala kuoneshwa makaburi Yao kila nilipokua namuuliza baba makaburi ya mababu zetu yako wapi alikua ananiambia yapo kijiji cha pili ipo siku nitawapeleka lakini hajawahi kutupeleka mpaka leo hivyo hivyo kwa baba zangu wakubwa na wadogo hawakuwahi kuwapeleka watoto wao abadani, kimafanikio kielimu na kiuchumi kwenye Familia yetu hakuna kabisa katika watoto wa babu mtoto wake wa kwanza tuu ndio alipata degree miaka hiyo na alikua mwalimu wa kahororo huko bukoba lakini hakukaa sana alikuja kufa kwa ukimwi wa miaka Ile, baba zangu wakubwa na wadogo maisha Yao wote ni ya dhiki tuu.
Ukija upate wa sisi watoto hivyo hivyo kielimu ni kawaida sana Kuna mtoto wa baba mdogo ndio Ana degree ya ualimu ila maisha yake ni Yale Yale, ukoo wetu ni mkubwa sana wametapakaa kila sehemu ila kila mtu na maisha yake baadhi ya ndugu zangu siwajui tumelelewa bila umoja yani sisi wajukuu hatujuani wazazi wetu hawana umoja kabisa hivyo kupelekea sisi kutojuana baadhi ya wajukuu hata huko kijijini hawajawahi kwenda kabisa.
Turudi kwenye Familia yangu, Dada alimaliza advance akaenda chuo akasomea mambo ya uhasibu ila hakupata kazi Sasa ameolewa geita, Dada yangu mwingine yeye aliishia form 3 akapewa mimba anatangatanga tuu kazalishwa watoto wanne baba tofauti kwa Sasa yupo mbeya anauza bar, mimi nilifika mpaka advance ila sikupass vizuri nikaenda college nikasomea mambo ya afya ila nilipofika mwaka wa mwisho niliacha chuo mwenyewe mpaka Sasa sijui sababu ya kufanya hivyo ilikua ni nini.
Nimeshafanya biashara nyingi ila sifanikiwi kamwe nimezunguka mikoa mingi kujitafuta ila bila bila kila ninalofanya halifanikiwi nimesali sana na kufunga ila wapi, nimeshaomba sana kazi nyingi zisizo na taaluma ila nikiitwa tuu kuanza kazi siku mbili nyingi naachishwa bila sababu ya msingi nikiuliza tatizo nini naambiwa nenda tutakuita, nikaamua kwenda kusomea udereva nikapata lesseni lakini kazi sipati.
Nikakutana na mzungu mmoja wa Canada tukawa washkaji akaniambia nitafute passport aje anifanyie mpango niende Canada nikapige kazi nikapamba sana nikaipata ila nilivyomcheki akaniambia nisubiri ni miaka Sasa mpaka nishakata tamaa na maisha.
Nilikua nakaa dar es Salaam miaka ya nyuma nilipomaliza chuo nilamua nianzishe biashara ndogo huko ila ilikuja kufilisika nikaamua kukimbilia mikoani kujitafuta ila Hali bado tete hapa nilipo nipo kwa Dada yangu mkubwa yani kwa shemeji yangu umri wangu ni miaka 30.
Sina future nishapoteza matumaini Kote naona giza umri unaenda nilichonacho ni kitanda na godoro pamoja na redio niliviacha dar es Salaam na hapa mkononi Nina balance ya laki 5 tuu ndio imebaki baada ya kuyumba kwenye biashara ya samak sijui nifanye nini naogopa kuchoma tena haka ka balance kwasababu Sina backup yoyote.
Kuna jamaa nilikutana nae nikamueleza historia yangu akaniambia nirudi kwa mababu(MIZIMU) niililie eti imekasirika kisa tumeitenga bila hivyo nitateseka maisha yangu yote nikaona nije niwashilikishe pia je niende nikaililie mizimu? Kuhusu kusali nimesali sana but it doesn't work to me anymore Kuna mchungaji aliniambia inabidi nisali sana nijitenge na madhabau ya mizimu nilisali sana na kufunga sana ili sioni chochote.
Najua humu Kuna watu wanaoweza kunisaidia kiushauri naomba ushauri wenu nawaza sana juu ya hatma ya maisha yangu, humu Kuna watu mna biashara zenu zimesimama vizuri tuu kama Kuna mtu anaweza kunipush kwa kuniconnect na biashara yake kulingana na mtaji wangu nitashukuru pia kama naweza kuelekezwa niende wapi nikaangalie kwenye kilo nipo tayari pia, kama Kuna kazi yoyote naweza kupata nipo tayari pia ndugu zangu naombeni msaada. Mtanisamehe kwa uandishi m'bovu. Mchana mwema.