Nipo Tayari Kuitumikia Jamii

Nipo Tayari Kuitumikia Jamii

Joined
Jul 31, 2024
Posts
11
Reaction score
21
Kama kijana ambaye bado najitafuta ili kujiboresha na kufikia malengo yangu, naomba kutumia jukwaa hili kutafuta mtu ambaye anaweza kunishika mkono au kuwa daraja kwangu la kunivusha kutoka hapa nilipo na kunipeleka kwenye hatua inayofuata ya maisha yenye nafasi na mafanikio zaidi. Ninatafuta ushauri, connection, au hata nafasi ya kazi ambayo inaweza kunisaidia kujenga maisha bora.

Ninatafuta nafasi ya kazi inayoendana na ujuzi na uzoefu wangu. Umri wangu ni miaka 26 kiwango changu cha elimu ni Astashahada katika Teknolojia ya Ufugaji Samaki (Diploma in Aquaculture Technology and Aquatic science) na nina uzoefu wa miaka miwili kama msimamizi na muendeshaji wa miradi ya ufugaji samaki. Aidha, nimekuwa Afisa Masoko na Muandaaji wa Maudhui katika sekta ya utalii, pamoja na uzoefu wa mwaka mmoja kama Meneja wa Baa.

Nina leseni ya udereva na ujuzi mzuri wa kutumia kompyuta, hasa programu za Microsoft Word na Excel. Mimi ni mchapakazi, rahisi kufundishika, na nina uwezo wa kuadapti mazingira mapya haraka.

Lengo sio kutafuta huruma, binafsi ningependa kupata nafasi ya kazi yoyote inayopatikana kutokana na sifa zangu na uzoefu nilionao. Naamini kwamba ninaweza kutoa mchango mkubwa kwenye majukumu yoyote nitakayopangiwa na kuleta mabadiliko chanya.

Kwa yoyote aliyoguswa na mwenye nia ya kunisaidia tafadhali wasiliana nami kupitia [0621903381] au PM.
Asante kwa kuzingatia ombi langu.

“We rise by lifting others”
 
Wewe ni Mr au miss
 
Habari za majukumu wakuu

Mimi bado nina hustle sijapata kazi, kama kuna mtu yoyote anaweza kunishika mkono mlango uko wazi

Kwa sasa hivi nipo Mwanza
 
Back
Top Bottom