Nipo tayari kuingia sasa

Manun'guniko

Senior Member
Jul 23, 2014
155
59
Habar zenu waAfrika kamili.

Kwa kifupi mimi ni mzima kabisa yaani sijui niseme nini kwa kweli nashukuru kichwa kimepona japo kilikuwa kinauma kwa mbali.

Sijaja humu kwa salamu tu kwa sababu nitaishia kukosolewa lengo kuu ni kuhusu mahusiano nilikuwa naogopa kuingia katika mapenzi kwa sababu yameumiza asilimia kubwa ya watu sasa nimen'gamua akili yangu na sasa nipo tayari kuingia katika mahusiano sasa jambo la msingi nataka tuwe pamoja katika ushauri pale nitakapoleta uzi wa masikitiko na wa furaha.

Kwasababu kuna watu wameshaanza kuninyemelea najua kuna wakweli na waongo niombeeni nisilie kama watu wengine bali niwe nafuraha katika mapenzi kama baadhi ya watu wengine.

Haya jamani nimemaliza sitaki kukosolewa na kukosolewa ni vibaya sana

Nawapendeni wote japo siwajui.
 
Ndo jiandae kwa yote pia. Kuna siku za kulia na za kucheka pia. Kila la kheri

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
PICHA? sijasema natafuta mpenz humu jf nataka ushaur sitak kujidanganya humu
 

Hongera sana. Nawe uwe Tayari kukabiliana na mazuri na mabaya yatakayojitokeza ili mwisho wa siku uufurahie ushindi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…