Nipo dilema: Je, niuze pikipiki yangu Boxer BM 150 ninunue Shineray inayotumia umeme?

Alejandroz

JF-Expert Member
Feb 14, 2017
327
376
Habari great thinkers

Nina boxer bm 150 niliyoitumia kwa takribani miaka 7 (84,000km mileage) sasa kuna mtu katokea anaitaka kwa 1,700,000/=

Sasa nilikuwa nafikiria nikiuza ninunue Shineray (1,400,000) yenye shape ya "Scooter" ya kuchaji maana naona ni economy kwenye suala la fuel

Sio mtu wa masafa kiivo mishe zangu ni hapa hapa mjini,, Sasa changamoto ya hizi Shineray ni speed haizidi 50km/h ila ukiicharge full ni umeme wa 400Tshs (kwamasaa 6) baada ya hapo inatembea 60 km hadi kuicharge tena

Sasa nipo dilema je niuze hii Boxer au niache,, naomba ushauri wako mwanafamilia mwenzangu
 
Vpi kuhusu gharama za mafuta na charge mkuu?
Binafsi ninaipenda sana boxer yangu bm 150 Ina nguvu popote itume inafika kuhusu mafuta sio sana ni kawaida tu labda kwa kuwa sijawahi kumiliki pikipiki aina nyingine tofauti na hii lakini mie naitumia kwa matumizi yangu binafsi na sio bodaboda hivyo mara nyingi nipo makini kwenye service na matengenezo mengine madogomadogo kuhusu hivyo vya kucharge naona hivyo luxury sana halafu havina speed unapobidi kwenda speed lakini naona kana advantage ndogo kuliko disadvantage
 
Vipi gharama za uendeshaji mkuu
Hakuna kisicho na gharama hapo.Na ukitaka sana vitu rahisirahisi kuna gharama pia.Boxer utaitumia muda mrefu kwa kazi/huduma ngumu na nyingi.Wakati scooter utatumia gharama ndogo ila haidumu muda mrefu(enduro/durable) kila muda mfupi utatakiwa ununue vifaa au yenyewe mpya.Chagua.
 
Back
Top Bottom