Niombe Talaka?


Kama ni ndoa unayoweza kuomba talaka inamaanisha unaweza kuolewa tena, fanya hivyo. Kama ni ndoa ya kifo kiwatenganishe usiondoke humo ndani ila badili jinsi ya kuishi kidogo tu.. mfanye kama picha, uambie moyo ufe ganzi baki ndani kwa ajili ya wanao mfanye kama anavyokufanya wewe, jicho kwa jicho.
 

wanafikiri watoto hawaoni au hawaelewi. mimi nakumbuka incident imetokea nina miaka 7!! nilijua kuna tatizo na nilijua wanafikiri sijui. toka siku ile ni kuwafuatilia tu. all my life nimefanya kazi ya uSpy kumlinda mama yangu. na nimetokea kumchukia baba.

SAY NO TO DOMESTIC VIOLENCE.
 

Nyie wa namna hii HATUNA JINSI MPIGWE TUU mwanamke kama wewe unakuwa na GUBU utafanyajwe zaidi ya kipigo.
 
Watu wameacha sana mafunzo ya dini na hili ni tatizo litakalosumbua sana katika ndoa. wanawake wanataka haki sawa jambo ambalo haliwezekani hadi kiama... Mungu hakosei.

WAEFESO 5
21 Enyi wake, watiini waume zenu kama kumtii Bwana wetu.

22 Kwa maana mume ni kichwa cha mkewe, kama Kristo naye ni kichwa cha Kanisa; naye ni mwokozi wa mwili.

23 Lakini kama vile Kanisa limtiivyo Kristo vivyo hivyo wake nao wawatii waume zao katika kila jambo.

24 Enyi waume, wapendeni wake zenu, kama Kristo naye alivyolipenda Kanisa, akajitoa kwa ajili yake;

hiyo ni bible....

Qur'an nayo..... ((Wanaume ni wasimamizi wa wanawake, kwa kufadhiliwa na Mwenyezi Mungu baadhi yao juu ya baadhi, na kwa mali yao wanayoitoa. Basi wanawake wema ni wale wenye KUTII na wanaojilinda hata katika siri kwa kuwa Mwenyezi Mungu Ameamrisha wajilinde..........)) [An-Nisaa: 34]

yani hii kitu haikwepeki ndivyo ilivyo na ndivyo itakavyokuwa.

kweli tumeona mtoto amelia kwa masaa mawili, lakini mama hajatuambia wakati anahesabu masaa ya mtoto kulia alikuwa anafanya nini? je walikuwa wako sawa na mumewe? ni usiku labda mumewe alitaka jimai akakataliwa kwa kusimangwa na matumizi ya asilimia 90, je kama mke anafanya kazi ana pesa haifai kumlea mume na watoto WAO? akiumwa haendi kazini nyie akina housegirl mtamtunza kweli kwa hali hii? pamoja na yote haya mmeona maneno aliyomuambia mumewe ni maneno sahihi ya kumuambia mumeo?

tumeambiwa tabia za mume kuwa siyo mlevi ni mkorofi, mbishi blah blah.... je tabia ya huyo mke ni ipi? kama ukorofi wa mume unasababishwa na ujeuri wa mke tutafika??

siafikiani kabisa na suala la kupigwa au kunyanyaswa kwa mwanamke, ila mjue kuwa wapo wanaume wepesi kupiga japo watajutia lakini washatoa kipigo, na mke mwenye mdomo ndo hupigwa zaidi kwa sababu kuwa na mdomo kwa mume huo siyo UTIIFU.
 
usiombe talaka...

what you need is TO GROW UP........
Grow up! How???kulea mtoto ni jukumu la baba na mama. sema ana mchepuko ndio maana anatoa vitisho' wanaume mmezidi'
 
Ndoa ni taasisi ambayo ni complicated sana, na huenda ndiyo maana tunatangulia kupewa Vyeti kabla, vingetolewa baada ya Ku practice graduates wangekuwa wachache sana.
 
Maelezo yoote hayo ni najibu ya swali la upande mmoja, akija nae me hapa na maelezo yake ndipo tutatia akili.
 
Ujihudumie mwenyewe, unyumba hupati, ukorofi na kuumizana roho....unashida nae wa nini.... acheni kung'ang'ania ndoa.....sorry my lady.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…