Nini umuhimu wa mashirika haya? TBS, TBC, TMA, BASATA

Kiparuanda

JF-Expert Member
Jul 23, 2013
1,578
2,377
TMA: Hii ni mamlaka ya hali ya hewa Tanzania, hawajawahi kuripoti ujio wa janga lolote la kiasili zaidi ya kutangaza daily kuwa kutakuwepo na mawingu, mvua, ngurumo na vipindi vya jua nchi nzima? (wakitambua moja ya hivyo lazima kitokee nchini siku husika). Kwa nn serikali isiombe raia mmoja ajitolee kufanya kazi hiyo bure?

TBS: Shirika la viwango Tanzania. Kwanini serikali inawajengea watu maofisi makubwa na kuwapa magari na mishahara wanapiga mishe za quality control wakati almost every comodity imported in this country is fake? Sio electronics, sio nguo, sio dawa, sio taaluma. Mtanzania unanunua pkpk mpya karibu sh 3,000,000 ina tbs ukijishau ikianguka hata kwa bahati mbaya inapasuka yote. Unaenda dukani unanunua vifaa vya umeme vina tbs unafanya wiring ukikaa mwaka mmoja vinapukutika. Pia kwenye bomba, bati, rangi, vioo, tiles, vitasa napo ni vivyo hivyo, haijalishi vimezalishwa tanzania au nje.

BASATA:Baraza la sanaa Tanzania. Kwanini wasanii wanalalamika kudhulumiwa haki zao wakati chombo hiki kipo? Wakina diamond wanafanya juhudi binafsi kulinda milki za kazi zao wakati hawa jamaa wapo bize kusikiza nyimbo za Ney wa mitego na snura bila kujali kuna wengine wanaonajisi maadili kwa kucheza ponografia kwa kisingizio cha music videos na wengine kuimba upumbavu kama hainaga ushemeji.

TBC: Tangu nikiwa chekechea maiaka ya 90 kuna babu namsikiaga akitajwa kama fundi mitambo (jina namsitiri), nashindwa kuelewa ni mitambo gani wanayomiliki hawa huku matangazo yanasua sua, hawana content ya maana, habari zao za uongo, poor reception, miziki ya zamani (japo mizuri, ila wamezidi). Hili naomba lifutwe, wafanyakazi wastaafishwe na majengo yabomolewe kabisa tuachane na hii biashara.

Hayo ni maoni yangu, tema povu tukabiliane.
 
umuhimu uliopo ni kwamba watu wamepata ajira kupitia hayo mashirika.
 
Kila MTU ana uhuru Wa kutoa Mawazo kwa mujibu Wa katiba ya JMT. Ila binafsi napenda ufanye utafiti au fuatilia jambo kwa undani kabla ya kutoa hitimisho LA jumla. Nikupe mfano Tu Wa majukumu ya Tma ni mengi shida huenda wewe ni mmoja Wa wale ambao huenda TV zao special kwa kuangalia miziki tena ya singeli ukiona taarifa ya habari unahamisha. Moja ya jukumu LA TMA ni kutoa utabiri Wa njia ya kila ndege iendako (flight enroute forecast) . Hii document anapewa rubani masaa mawili kabla hajaruka ajue hali ya hewa kwa njia yake na kiwanja aendacho (for safety of aircrft/passagers, load and fuel consumption planning). Umewahi kujiuliza kwa nini ajali za ndege ni chache sana duniani? Waongoza ndege wote duniani humweleza rubani hali ya hewa ya Kiwanja anapotaka kuruka au kutua. Hivi ulishawahi kupanda ndege na kubaki hewan kwa muda kwa ajili ya hali mbaya ya hewa? Basi tambua kuwa anaetoa ushauri wa ile ndege itue au ikatue uwanja mwingine ni ofisa hali ya hewa wa zamu kwa kumshauri airtraffic controller kwa kutabiri urefu wa kipindi cha hali mbaya ya hewa. Kama una nduguyo pilot muulize umuhimu Wa weather atakuleza. Meli zote ziendazo Zanzibar huchukua Document maalum toka ofisi ya hali ya hewa bandari dar/ znz yenye kuonesha nguvu ya upepo baharini na kina cha mawimbi ili kulinda usalama Wa chombo, Mali na maisha ya abiria kama ilivyo kwenye ndege. Huo utabiri unaobeza kuwa ni mawingu nchi mzima uliuona wapi? Tena Siku hizi utabiri unawekwa hata kwenye page ya Facebook ya TMA pitia uone acha Ku.assume. utabiri Wa hali ya hewa wa upo wa masaa 24, Wa mwezi, Siku kumi (decadal forecast), wa msimu Nk. Na kila
mmoja una matumizi yake.
Kuna utabiri maalum kwa ajili ya shughuli za kilimo(agrometeorological forecast) maafisa kilimo huutumia sana kwa ajili ya kutoa ushauri aina gani ya mbegu mkulima apande (short or long variety), kujua kiwango cha maji ardhini. Kuna wataalam Wa hydrology (hydrometeologist) ambao wanashirikiana kwa karibu sana na wizara ya maji na dawasco. Kuna utabiri maalum kwa ajili ya eneo LA Ruvu ambako ndiko maji ya kunywa kwa watu Wa dar yanatoka. Nisikuchoshe
kumbuka wahenga waliogopa umande lakini kauli zao bado zinaongoza maisha ya wasomi na moja kati ya hizo ni hii JAMBO USILOLIJUA NI USIKU WA GIZA
 
Back
Top Bottom