Msigazi Mkulu
JF-Expert Member
- Dec 22, 2013
- 4,110
- 3,269
Nina jihisi nina hili tatizo maana nikiwa kwenye vyombo vya usafiri watu ugaeuzia shingo zao pande mwingine na wife hawezi lala tumetazamana. Nilichukua hatua ya kwenda hospitali mara mbili tena kubwa nikiwaeleza nina tatizo la kutoa harufu mbaya mdomoni mara zote madaktari wa meno wameniambia sina hilo tatizo na kuishia kunipa mouthwash na mimi nimekuwa nikizitumia mara kwa mara bila kupona. Sasa katika uchunguzi wangu nimegundua kuna baadhi ya watu hasa huku kanda ya ziwa wanatoa hizo harufu puani na kali sana pamoja na mimi kuwa na hilo tatizo lakini hujikuta nikikaa karibu na watu wa dizaini hiyo huwa nakwepa kugeukia upande walipotazama. Hili tatizo wanalo watu wengi hasa huku kanda ya ziwa. Nini chanzo chake na tiba.