Nini maana ya utu wa binadamu?

God'sBeliever

JF-Expert Member
Joined
Sep 1, 2015
Posts
5,786
Reaction score
3,068
Habari za jioni wakuu, natumai shughuli ilienda na inaendelea vizuri kwa wale ambao haijaenda sawa basi yote shukuru kesho pambana utafika.

Naombeni mnielezee nini thamani ya utu wa binadamu kwanza I feel tortured……
******************************************************************************

Nimekua nikipitia matatizo mengi sana hali iliyonifanya niachane na mfumo wangu wa maisha na kuishi tofauti. Leo ngoja niongee na ndugu zangu maana huwa siweki chuki moyono bali tunasahihishana wote mwisho wa siku peace na love kama kawaida.

Ndugu zangu ugomvi wangu na nyinyi umeanza lini? Wapi nilikosea namna hii? Kwa nini usiniite tukae tuongee tuyamalize mwisho wa siku kila mtu akatafte rizk apate kuishi? Ya nini kila siku waitesa nafsi yangu? Kwa baya lipi nililotenda? Kuokoa watu, kufata ninaloliamini au kusaidia watu? Wengine wamefikia hatua ya kulaumu kabisa kwanini sipatwi na mabaya badala yake nazidi kufanikiwa? Real? Roho yangu mbaya ni ipi? Embu nitajie hayo maasi niliyofanya hadi kufikia hiyo level nami nitubu basi. Taabu nipatazo nimegeuka kuwa mbaya tena?

Binadamu unaweza kujiona we ndio mfalme katika hii dunia kwamba una access na maisha ya binadamu lakini kimsingi we sio kitu bali Mungu aliekuumba wewe ndio ana mamlaka na wewe. Kama Mungu alikuumba kwa jambo fulani basi utalitenda tuu pasipo vitisho wala dhihaka za binadamu.

Leo hii wanidhalilisha, waniwinda kama mnyama yote haya sababu ya nini? Ni hizi mali za kidunia? Basi mimi sizihitaji wala sijawahi kuzifikiria na mimi niko hivi nilivo wala sitakaa nipumbazwe kamwe kwa sababu najitambua vyema na yote namuachia mwenyezi Mungu maana yeye ndie mtenda haki wala sio vitisho vya binadamu. Wengine wakaenda mbali zaidi nikianguka kimasomo inakua furaha kwao sawa ila mwisho wa yote kila mtu atavuna apandacho na ndipo ulimwengu utatambua yote yatavunwa hapa hapa duniani tuu. Wengine wakaona haitoshi wakaanza kuniwekea vikwazo kwenye academic issues, wengine waka deal na mitandao ya kijamii bado tuu nyngine waka hack kabisa na kama haitoshi wakaweka hata ID zetu public! So you though I was looking for popularity? Dumping you and the rest ni dharau? Mnajua kila mtu ana misimamo yake? For the sake of what? Kuna siku mtajibu haya in voice of holly bible not me and you aware with it!

Una weka mawasiliano yangu kwa watu na kunivua nguo yote haya kwaajili ya nini? Hata utu wa ubinadamu huna leo huelewi hata sisi hatuna mda na mambo yenu sasa yanini kupoteza mda wa watu? Jasho langu unajua nimelipataje? Kwanini mimi kila siku nionekane mbaya wakati mimi najifahamu sio mbaya bali mkimya? Imefikia stage naitwa fisi, mbwa mwitu, shoga, mpenda damu, roho mbaya kwa ajili ya kitu gani nilichofanya? Hivi mnajua kuna siku mtajibu haya mbele ya mwenyezi Mungu? Mtajibu nini siku ikifika? Mnadhani hata ile pumzi ya mwisho hizo nguvu zenu mtakua nazo sio? Basi Mungu sio athmani halijawahi kumwagika chozi la mtu bure Mungu pia hutujalia sisi wanyonge.

Kwani binadamu alipojitambua na kuvaa nguo kusitiri uchi wake hakuwa sahihi? Sasa kwanini nyinyi msijali haki za binadamu? Thamani ya ubinadamu hamuijui? Mpaka damu ya mtu imwagike ndio mtaridhika sio?

Watu tuna maisha ya dhiki hela zenyewe za mkopo tumepata kwa bahati tunajitahidi tuje kukomboa familia zetu nyinyi hamjali hili sasa sijui mna mioyo ya kibinadamu au hamna miili ya nyama na damu hivo hamsikii uchungu wa kilio changu. Lakini na nyinyi simpo/mlipita humu hata kama mlikua na hali nzuri ya nini kunyanyasa maskini? Sasa mimi nitapataje kazi wakati mmenifanya nisisome? Halafu eti mnasema Tanzania hamna wasomi wakati nyinyi ndio mmesababisha yote haya? Do you think you are right? Okay we still have hope, one day God will say no to all bullshit! And will answer to all depressed individuals and refine them too. Psalm 34:12-22.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…