Nimekuwa najiuliza nini maana ya kuitwa au kuwa Baba
Je, ni kuzaa mtoto au watoto na kuingia mitini na kumuacha Mama akitaabika?
Je, ni kuzaa mtoto au watoto na kuwalea kwa pamoja na Mama (Mke)?
Je, ni kuzaa uko mtaani kwa wanawake tofauti na kujitangaza kidume kwa kuwa umeweza kuzaa na wanawake tofauti?
Nimeweka hii mada hapa kwani nina mshikaji wangu ambaye Baba yake baada ya kuzaa na Mama yake walitengana na mshikaji kukulia kwa ndugu wa Mama na Mungu saidia amesoma mpaka chuo. Sasa ndugu wa Baba wanaanza kumfuata na kumwambia mjali Baba yako, maisha yake sio mazuri kwa sasa vinginevyo utapata laana kutoka kwa Baba yako. Halafu kumbuka mshikaji toka chekechea hadi anamaliza chuo mwaka jana hajawahi kukutana na Baba yake. Ila msimamo wa mshikaji yeye ni kuwa kwa mateso aliyopata kwa kuishi kwa ndugu mara uku mara kule halafu uishi kwa uhuru kama nyumbani vile kumemfanya amchukie Baba yake na anasema kamwe hamfikirii hata kidogo kwenye maisha yake. Ameamua ni yeye na Mama yake na ndugu za Mama yake Kwani ndio wanajua uchungu na mateso ya kumlelea mpaka hapa alipo leo.