Ahsante Doctor kwa majibu yako mazuri.Unapojigonga unasababisha "trauma" kwenye seli, yani unaziumiza hivyo zinarespond kwa kutoa vichochezi viitwavyo cytokines ambavyo husababisha yafuatayo
1.Kutanuka kwa mishipa ya damu kwenye eneo husika hivyo kusababisha eneo kuwa jekundu na lenye joto hata kabla ya kuvimba kutokana na mrundikano wa damu eneo hilo
2.Baadhi ya vichochezi "cytokines" kama histamine husababisha kuongezeka kwa uwezo wa kupenyesha vimiminika "permeability" katika kuta za mishipa midogo ya damu ya eneo hilo inayoitwa kapilari hivyo kimiminika kiitwacho plasma hupenya kutoka kwenye damu na kuingia kwenye vijinafasi kati ya seli na seli "intercellular spaces" hivyo mrundikano wa kimiminika katika vijinafasi hivo husababisha UVIMBE kwenye eneo husika.
2.Pia baadhi ya vichochezi vinavyozalishwa kama Bradykinin ndivyo husababisha maumivu.
Yangu ni hayo tu naamini umenipata
Safi.Unapojigonga unasababisha "trauma" kwenye seli, yani unaziumiza hivyo zinarespond kwa kutoa vichochezi viitwavyo cytokines ambavyo husababisha yafuatayo