Heading yako haipo sawa. Unafahamu chuo cha taifa wewe?.
kwenye vyombo vya habari waliandika chuo kikuu. that was specific. udsm. kama ingekuwa tumaini au udom wasingesema chuo kikuu. bali chuo cha.... fill in da blank. sio dharau mkuu ni mazoea tu. teh teh
Heading yako haipo sawa. Unafahamu chuo cha taifa wewe?.
ndio,
ni Chuo chenye sura ya kitaifa, yaani uwezo wa kuchukuwa idadi kubwa ya wanafunzi kwa kozi nyingi iwezekanavyo, na kiwe kinamilikiwa na serikali kwa asilimia zote bila kusahau kuwa tegemeo la taifa kitaaluma.
Therefore UDSM qualifies to be a State University.
Au wewe una maoni gani?
kwani kuna kingine zaidi ya udsm?
nipe vigezo vya kukipa udsm hadhi ya chuo cha taifa.
Hajui huyu hata upeo wake wa kufikiri ni mdogo sana. Hajui hatma yao ni kupoteza mwelekeo wa kimaisha kwani hilo ndo lengo kuu la Serikali ya CCM, Kwa mtu yeyote ambaye anamtazamo tofauti na CCM.Heading yako haipo sawa. Unafahamu chuo cha taifa wewe?.
hapana mkuu.
Michango ya akina mzee ndo imechafua thread... Mimi nina lengo zuri la kujua hatima ya wanafunzi hao 41 walioshtakiwa Kisutu Magistrate Court...
nakushauri uwe unahudhuria kesi zao pindi zinapotajwa
Heading yako haipo sawa. Unafahamu chuo cha taifa wewe?.
humu ndani mada imeshawekwa pembeni sasa na kuanza mabishano ya vyuo maana kuna wengine bila ubishi kati ya UDOM na UDSM siku haiwi nzuri
Hawa ni wale waliofukuzwa Chuo Kikuu cha Kata ya Ubungo, kutokana na kufunguliwa mashtaka na Jamhuri kufuatia mgomo wa tar 11 Novemba 2011.
Majuzi nilionana na wawili kati yao, wakaniambia kuwa kuna michakato ya kisheria wanaifanya kupinga kufukuzwa kwao kwa hisani ya Prof. Shivji, na kwa upande wa mahakamani, kesi yao ilitakiwa kusikizwa Jumanne ya tar. 20 Desemba 2011. Kutokana na mvua kubwa ya mafuriko, nikashindwa kufika Kisutu Magistrate hiyo saa mbili ilivyotakiwa, jitihada zangu zote za kusaka habari za kesi yao mtandaoni na kwenye magazeti zikakwama, kuwaona uso kwa macho ikashindikana kwa kuwa hawako tena shuleni, achilia mbali uwezekano wa kufutiwa dhamana waliyowekewa na ex-co-student wenzao wa UDSM, kwani sheria ndogo za chuo haziruhusu mwanafunzi kumdhamini raia kwa mgongo wa Afisi ya Mshauri wa Wanafunzi.
Kwa yeyote mwenye taarifa za mwendelezo wa kesi yao anifahamishe...
Natanguliza shukurani.