Watu hawana hofu ya Mungu kwa hiyo asilimia kubwa sana ya Watanzania ni wabinafsi. Kukosa hofu ya Mungu maana yake japo kila mtu ana dini yake na mbele ya watu anajifanya ni mcha Mungu sana lakini nyuma ya pazia hajali kabisa kama matendo yake yataumiza au hata kuua Watanzania wenzake. Haogopli kwamba iko siku ya hukumu mbele ya Mungu.
Hali hii si kwa viongozi tu bali ni kwa watu wa ngazi zote. Mwanakijiji wa hali ya kawaida akipewa pesa za kutosha yuko tayari kuficha na kuwezesha wageni ambao kesho wanaweze kuja kumdhuru yeye mwenyewe. Kiongozi anakubali dawa zilizoisha muda kuingia madukani bila kujali kwamba watoto na ndugu zake au hata yeye mwenyewe anaweza kuja kuzitumia zimuue. Viongozi wanapeleka watoto wao kwenda kusoma nje bila kujali shule za kata hazina walimu wala vitabu wala maabara. Hata viongozi wa dini ambao sisi tunawaona kama wacha Mungu wengi wao hawakemei maovu wakati yakitendwa na matajiri au viongozi wa kiserikali kwa sababu wanapokea misaada toka kwao. YOTE HAYO NI MATOKEO YA KUKOSA HOFU YA MUNGU